IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa / 26

Ukarimu na upendo katika Kisa cha Nabii Musa (AS)

20:15 - September 02, 2023
Habari ID: 3477535
TEHRAN (IQNA) - Chanzo kikuu cha nishati kwa wanadamu ni ukarimu, upendo na wema. Ni chanzo kisichoisha na hakuna kinachokitishia.

Ndiyo maana kuisoma katika njia ya elimu ya manabii ni muhimu sana.

Mbali na chakula, maji, hewa, n.k., mwanadamu anahitaji ukarimu na upendo. Ukarimu ni jambo linalowaunganisha watu na kujenga mshikamano miongoni mwao. Bila hivyo, hakuna uhusiano ambao ungeundwa kati ya watu, hakuna mtu ambaye angechukua jukumu la kuwajali wengine na hakungekuwa na kujitolea na hakuna usawa.

Nguvu ya upendo na huruma pia ni muhimu na yenye ufanisi katika elimu ya kidini. Ikiwa inatumiwa ipasavyo na kwa usawaziko, ingetimiza fungu kubwa katika kuwasaidia watu wakue kibinafsi na kiroho.

Aina bora ya elimu ni ile inayohusisha huruma na upendo. Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpamba Mtume wake kwa njia ya mapenzi na Mtukufu Mtume Muhmmad (SAW) alifaulu katika elimu ya dini ya watu kwa kutumia njia hii.

Umuhimu wa njia ya wema na upendo ni kwamba inaleta utii. Hiyo ni, wakati upendo wa mtu unaingia katika moyo wa mtu mwingine, angekuwa mtiifu na mfuasi wa mtu huyo.

Kwa hivyo hakuna njia yenye ufanisi na yenye manufaa kama njia ya upendo na huruma.

Nabii Musa (Amani ya Mwenyezi Mungu Iwe Juu Yake-AS-) alitumia njia hii kwa kuwaonea huruma na kuwarehemu watu wake sana.

Hata aliingia katika makabiliano na watawala wa wakati huo ili kuwaokoa watu wake.

Baada ya kuwaokoa Bani Israil, Musa (AS) alionyesha wema kwa watu licha ya malalamiko yao, akitafuta visingizio na tabia nyingine mbaya.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 86 ya Sura Taha:

“Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu na kusikitika. Akasema: Enyi watu wangu! Kwani Mola wenu Mlezi hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa muda mrefu kwenu au mmetaka ikushukieni ghadhabu ya Mola wenu Mlezi, ndio maana mkavunja miadi yangu? 

Alizungumza na watu wake kwa ukarimu na huruma ili kuimarisha uhusiano wa karibu na wa kindani pamoja na watu.

captcha