IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa/18

Ibtila katika kisa cha Nabii Musa (AS)

15:40 - August 08, 2023
Habari ID: 3477399
TEHRAN (IQNA) – Musa (AS), ambaye alikuwa nabii ni Ulul Adhm yaani ni miongoni wajumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye jina lake limetajwa katika aya nyingi za Qur'ani Tukufu, alitumia njia ya muhimu ya kuwaelimisha Bani Isra’il ambapo watu huwekwa katika hali fulani ili utayari wao wa kuendelea na njia uweze kutathminiwa.

Njia hii ni Ibtila, neno la Qur'ani Tukufu linalomaanisha kubadilisha hali za mtu kwa amri ya Mwenyezi Mungu ili talanta yake iweze kukua na kupata nguvu katika njia ya kumtumikia Mwenyezi Mungu.

Tunapotaka kumwongoza mtu kwenye eneo la elimu, tunapaswa kutumia njia ili kuona jinsi alivyo tayari na kutayarisha njia ili asonge mbele kuelekea mahali hapo. Njia hii inaitwa Ibtila.

Ibtila sio tu kwa ajili ya kumjaribu mtu ili kutambua udhaifu na nguvu zake bali pia inasaidia kumtakasa na kumtia nguvu kwenye njia ya ukuaji.

Nabii Musa (AS) aliwaweka Bani Isra’il katika hali kama hizo ili kuzitakasa nafsi zao.

Mtu wa Bani Israil aliuawa. Hakuna aliyejua muuaji ni nani. Kisha kukatokea migongano kati ya makabila mbalimbali ya Bani Isra’il kuhusu suala hilo, kila moja likihusisha mauaji hayo na jingine. Hatimaye, walikwenda kwa Musa (AS) kwa ajili ya hukumu.

 Na Musa alipo waambia watu wake: Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mchinje ng'ombe. Wakasema: Je! Unatufanyia mzaha? Akasema: Audhubil lahi! Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni mwa wajinga. (Aya ya 67 ya Surat Al-Baqarah)

Wananchi walianza kutoa visingizio mbalimbali na kuuliza maswali yasiyo na umuhimu kwani huyu ng'ombe aweje, awe na rangi gani, awe mnene au mwembamba n.k.

Kwa sababu Bani Isra’il walikuwa wameishi Misri kwa miaka mingi, walikuwa wamekubali baadhi ya imani za Wamisri, kutia ndani imani kwamba ng’ombe ni watakatifu.

Kwa hiyo amri ya kumchinja ng’ombe ilikuwa Ibtila, iliyokusudiwa kuwasaidia kutambua kwamba ng’ombe si watakatifu.

captcha