IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa / 17

Njia ya Uliza Ujibiwe katika kisa cha Nabii Musa katika Qur'ani Tukufu

20:37 - August 06, 2023
Habari ID: 3477388
TEHRAN (IQNA) – Nabii Musa (AS), ambaye alikuwa miongoni mwa Ulul'azm Anbiya (Manabii Wakuu), alitumia njia ya kujibu maswali ili kufundisha watu binafsi na makundi mbalimbali ya watu.

Qur'ani Tukufu katika aya tofauti inaashiria matumizi ya mbinu hii ya kuelimisha.

Mbinu ya kujibu maswali ni nzuri sana katika kufundisha na ina ufanisi hasa linapokuja suala la kufundisha watu umma.

Katika njia hii, ili kumtia moyo mwanafunzi au yule anayefunzwa, tuna mpa motisha kuhusu swali alilouliza na kisha kumpa maelezo.

Kitu kinapowasilishwa katika msingi wa Fitra au maumbile asilia mwanadamu huwa hana budi ila kukikubali.

Baadhi ya mifano iliyotajwa ndani ya Quran ambamo Musa (AS) anatumia njia hii ni hii ifuatayo:

  • Firauni alitaka kumfunga jela Musa (AS) kwa kosa la kumuamini Mungu Mmoja. Musa (AS) akamwambia: "Itakuwaje kama nitakuletea uthibitisho ulio wazi (wa kuwepo kwa Mungu)?" (Aya ya 30 ya Surat Ash-Shu'ara). Alimuuliza Firauni swali hili kama angesisitiza kukanusha kuwepo kwa Mungu na utume wa kinabii wa Musa na kumfunga jela hata kama atamuonyesha ushahidi. Firauni aliona ukweli lakini akaanza kutoa mashtaka dhidi ya Musa.
  • “Na mwambie: Je! Unataka kujirekebisha?” (Aya ya 18 ya Surah An-Nazi’at). Hapa Musa (AS) anataka kujua iwapo Firauni anakusudia kuacha ukafiri na ukandamizaji na kuanza kumwamini Mungu. Jambo tunalopaswa kujifunza kutokana na aya hii ni kwamba tunapowaalika na kuwaelimisha watu, tunapaswa kutumia maneno mazuri na yenye kuvutia na kuwatia moyo kuukubali ukweli. Firauni, hata hivyo, hangekubali. Alikataa mwaliko wa Musa na kuendeleza uasi wake dhidi ya Mungu.
  • Qur'ani Tukufu pia inazungumzia jinsi Musa (AS) alivyowaokoa Bani Israil na jinsi walivyomwomba baadaye awafanyie miungu kama miungu ya waabudu masanamu. Musa (AS) akawaambia: Je! nikutafutieni mungu yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu? Amekutukuza juu ya mataifa. (Aya ya 140 ya Suratul A’araf). Kwa hakika, katika maswali yote haya ambayo Musa (AS) aliuliza, nia ni kuamsha upande mwingine na dhamiri zao, na baada ya hapo wanapata uwezekano wa kuchagua njia sahihi inayoongoza kwenye wokovu. Bila shaka, baadhi ya watu hujihusisha na dhambi kiasi kwamba dhambi hupunguza athari ya Fitra katika maisha yao. Ndio maana Firauni hakubadili njia zake na akaishia kwenye adhabu ya milele.
captcha