IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa/ 23

Tawbah Inatumika Kama Njia ya Kielimu

21:06 - August 26, 2023
Habari ID: 3477500
TEHRAN (IQNA)- Njia ya kielimu yenye ufanisi zaidi ni ile inayomtia moyo mtu kutoka ndani kuelekea kwenye wema na kujiepusha na maovu.

Tawbah (kutubia) ni njia kama hiyo. Tawbah maana yake ni kujuta kwa kufanya dhambi, kuamua kutolitenda tena na kufidia dhambi uliyoifanywa. Kwa mujibu wa Uislamu Tawbah maana yake ni kuacha dhambi, kujuta, kuwa na nia ya kutorejea kwayo, na kuandaa mazingira ya kutorejea kwayo.

Masharti haya manne yanapotimizwa, msingi umewekwa kwa ajili ya kutorudia dhambi.

Tawbah ni njia ya kipekee ya kukaa mbali na maovu na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu. Kama njia ya Tawbah isingekuwa wazi, mwanadamu asingepata fursa ya kukua.

Tawbah ni njia ya kielimu inayomwita mtu kutoka ndani kuelekea kwenye wema na kurejea kutoka katika maovu.

Katika Aya ya 82 ya Surah Taha, Mwenyezi Mungu anawahutubia Bani Isra’il: “Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anaye tubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka."

Katika kisa cha Musa (AS), baada ya Mwenyezi Mungu kuwaokoa Bani Isra’il kutoka kwa Firauni na watu wake, Bani Isra’il walianza kuabudu masanamu wakati Musa (AS) alipokuwa mbali. Musa (as) aliporejea kwa watu, “Musa aliwaambia watu wake, ‘Na Musa alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Hakika nyinyi mmezidhulumu nafsi zenu kwa kuchukua kwenu ndama (kumuabudu). Basi tubuni kwa Muumba wenu na ziueni nafsi zenu. Haya ni bora kwenu mbele ya Muumba wenu. Naye akapokea toba yenu. Hakika Yeye ndiye apokeaye toba na Mwenye kurehemu.. (Aya ya 54 ya Surah Al-Baqarah)

Kuabudu ndama halikuwa jambo dogo baada ya Bani Isra’il kuona ishara nyingi za Mwenyezi Mungu na miujiza kutoka kwa Mtume wao. Walikiuka kanuni kuu za Tauhidi yaani kumuabudu Mungu Moja bila kumshirikisha  na wakawa waabudu masanamu baada ya Musa (AS) kuondoka kwa muda mfupi. Ndio maana Mwenyezi Mungu aliamrisha Tawbah na kurudi kwenye Tauhidi.

captcha