IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa /19

Muujiza Uliotumiwa na Nabii Musa kama mbinu ya kuelimisha

17:58 - August 12, 2023
Habari ID: 3477425
TEHRAN (IQNA) – Kuonyesha miujiza ni miongoni mwa uwezo maalum wa manabii wa Mwenyezi Mungu ambao una muelekezo wa kuelimisha au mafunzo.

Muujiza ni neno la Kiarabu linalotokana na mzizi Ajz (kutokuwa na uwezo). Muujiza ni kitendo ambacho wengine hawawezi kukifanya. Muajiza ni uthibitisho wa kauli ya Mtume kwamba ametumwa na Mwenyezi Mungu.

Muujiza ni jambo ambalo linafanyika kinyume cha mwendo wa kawaida wa mambo. Ijapokuwa katika baadhi ya nukta muujiza unashabihiana na uchawi na mazingaombwe n.k, lakini  tofauti kubwa ni kuwa Muujiza kamwe haushindwi kwani una asili ya Mwenyezi Mungu.

Mitume wa Mwenyezi Mungu walitumia miujiza kama njia ya kuwaongoza na kuwaelimisha watu si kwa ajili ya kuwaburudisha au.

Musa (AS) ni miongoni mwa manabii walioonyesha miujiza mingi katika maisha yake. Moja ya miujiza yake ilikuwa kuwashinda wachawi na waganga walioajiriwa na Firauni.

Siku moja kundi kubwa la watu lilipokusanyika mjini, wachawi walitumia uwezo na hila zao zote kumshinda Musa (AS). Walitupa fimbo na kamba zao chini na ikawa bahari inayowaka ya nyoka, wakipinda na kuteleza huku na kule.

Kwa muda, Musa (AS) alikuwa na wasiwasi kwamba watu wangewaamini wachawi na farao. Pia alikuwa na wasiwasi kwamba watu hawatatambua tofauti kati ya uchawi na miujiza.

Mara moja akaitupa fimbo yake na ghafla ikageuka kuwa nyoka halisi, akiwameza wale wengine wote waliodhaniwa kuwa nyoka.

Hapa, ukweli uliwekwa wazi kwa wote na wachawi walisujudu pale pale ili kukiri imani yao kwa Mwenyezi Mungu na kukiri kutokuwa na uwezo na kutokuwa na nguvu mbele ya nguvu za Mungu.

Kwa hiyo athari ya kielimu ya tukio hili iko wazi kabisa kwani wachawi mara moja walimwamini Mwenyezi Mungu.

captcha