IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa / 13

Kutumia kusababu katika njia ya kielimu ya Nabii Musa

18:41 - July 16, 2023
Habari ID: 3477289
TEHRAN (IQNA) – Hoja inayojumuisha kutoa hoja za kimantiki na zenye busara ni miongoni mwa mbinu za kielimu zenye nguvu na zenye ufanisi zaidi zilizoletwa kwa mara ya kwanza na manabii wa Mwenyezi Mungu.

Baadhi ya watu, wawe ni miongoni mwa waumini au la, wana fikra na mantiki kubwa katika dhati yao. Njia ya elimu inayotumiwa kwa watu hao haipaswi kuwa ile ile inayotumiwa kwa watu wenye mwelekeo wa kuwafuata na kuwaiga wengine bila kuhoji. Kutoa hoja ni njia ambayo kawaida hutumika kuelimisha na kufundisha kundi la kwanza.

Mwalimu mwenye uwezo wa kufikiri haogopi mjadala na maswali. Anawapa wanafunzi au wapinzani muda wa kutosha wa kutoa maoni yao na kisha kutumia sababu na mantiki kuwajibu.

Jambo lingine la kukumbuka hapa ni kwamba mwalimu au mzazi lazima azingatie umuhimu wa kukabiliana vizuri na makosa ya mwanafunzi au mtoto na kujaribu kurekebisha tabia zao mbaya kupitia njia zinazofaa. Hili likifanywa kwa njia mbaya na kwa njia zisizofaa, linaweza kuwa na matokeo na kuathiri vibaya akili ya mwanafunzi au mtoto.

Wakati mwingine mwalimu au mzazi hujaribu kumlazimisha mwanafunzi au mtoto kubadili tabia lakini kwa kawaida njia hii huishia kufeli na inaweza kusababisha tabia mbaya kuzidi.

Nabii Musa (AS), mmoja wa mitume wakubwa wa Mwenyezi Mungu, alitumia njia ya hoja katika kuwaelimisha watu.

Qur'ani Tukufu inasema: “Na mlipo sema: Ewe Musa! Hatuwezi kuvumilia chakula cha namna moja tu, basi tuombee kwa Mola wako Mlezi atutolee vile vinavyo mea katika ardhi, kama mboga zake, na matango yake, na thom zake, na adesi zake, na vitunguu vyake. Akasema: Mnabadili kilicho duni kwa kilicho bora? Shukeni mjini, huko mtapata mlivyo viomba. Na wakapigwa na unyonge,na umasikini, na wakastahili ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Na haya ni kwa sababu walikuwa wakiyakataa maneno ya Mwenyezi Mungu, na wakiwauwa Manabii pasipo haki. Hayo ni kwa walivyo asi na wakapindukia mipaka.” (Aya ya 61 ya Surah Al-Baqarah)

Katika aya hii, hoja imetolewa ili Bani Isra’il wabadili tabia zao:

1- Mahitaji yasiyo na mantiki ya mabadiliko ya chakula. Musa (AS) alijibu kwa hoja kwamba wasichague chakula kibaya zaidi badala ya kilicho bora zaidi.

2- Sababu za kuwadhalilisha Bani Israil.

A- Kukufuru, kuasi amri za Mwenyezi Mungu na kukengeuka kutoka kwenye tauhidi na kwenda kwenye ushirikina.

B- Kuua manabii wa kiungu na kupuuza amri za Mungu.

Hivyo, kama Bani Isra’il wasingefanya haya na badala yake wakatenda kwa mujibu wa amri za Mwenyezi Mungu, wasingekabiliwa na fedheha. Lakini hawakubadili tabia zao na hivyo kushindwa kufikia wokovu.

captcha