IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa / 15

Kujibari katika kisa cha Nabii Musa

20:28 - July 23, 2023
Habari ID: 3477326
TEHRAN (IQNA) – Kimsingi, mtu hawezi kuwa na mahusiano mazuri na ya kirafiki na watu wote. Hata mtu awe mzuri kiasi gani, atakuwa na maadui.

Kwa hivyo kuna sifa mbili ambazo zipo katika uhusiano wa watu: mapenzi na chuki. Sasa kigezo chetu kiwe kipi cha kuamua ni yupi tumpende na nani tusimpende?

Tawalli (mapenzi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) na Tabarri (chuki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) ni kanuni mbili muhimu za ambazo mtu anapaswa kuzitegemea katikak kuchukua misimamo ifaayo katika mahusiano na watu wengine.

Mtu anapaswa kuwa mwangalifu sana katika kuchagua marafiki na masahaba wake kwa sababu watakuwa na athari kubwa kwa tabia na mwenendo wake.

Tabarri, au Bira’at’, ina maana ya kukaa mbali na kitu chochote ambacho hakifai. Inamaanisha pia kuondoa kitu ambacho ni hatari.

Suala la Tawalli na Tabarri ni muhimu katika nyanja za kimaadili na kielimu kwani humsaidia mtu kukuza sifa nzuri za kimaadili katika tabia yake na kujiepusha na zile mbaya.

Imam Sadiq (AS) alimwambia mmoja wa masahaba wake aitwaye Jabir: Wakati wowote unapotaka kujua kama kuna wema ndani yako, angalia moyo wako. Ikiwa inawapenda wale wanaomtii Mwenyezi Mungu na kuwachukia wale wasiomtii Mweneyzi Mungu, wewe ni mtu mwema. Vinginevyo, wewe sio mwema na hakuna wema i ndani yako.

Nabii Musa (AS), ambaye alikuwa mjumbe mkubwa wa Mwenyezi Mungu, alimtumia Tabarri dhidi ya Firauni na watu wake.

Firauni aliogopa sana kwamba Tauhidi au itikadi ya Mungu mmoja inaweza kuingia kwenye kasri lake. Ili kuzuia hilo, aliamua kumuua Musa (AS). “ Na Firauni akasema: Niachieni nimuuwe Musa, naye amwite Mola wake Mlezi! Mimi nachelea asije kubadilishieni dini yenu, au akatangaza uharibifu katika nchi.” ( Aya ya 26 ya Sura Ghafir).

Musa (AS), ambaye inasemekana alikuwepo katika mkutano huo, hakuwa na hofu ya tishio hilo. Kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu, alisema: “Na Musa akasema: Mimi najikinga kwa Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi anilinde na kila mwenye jeuri asiye iamini Siku ya Hisabu." (Aya ya 27 ya Surah Ghafir)

Aliyoyasema Musa (AS) yanaashiria kwa uwazi kwamba wenye tabia hizi mbili ni watu hatari: 1- Ujeuri. 2. Kutoiamini Siku ya Kiyama.

Mtu anapaswa kukataa na kukaa mbali na watu kama hao na kukimbilia kwa Mwenyezi Mungu. Kuwa na kiburi husababisha mtu asione chochote na mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe na mawazo yake mwenyewe.

Kutokuwa na imani katika Siku ya Kiyama kunasababisha mtu hata kujaribu kusimama dhidi ya uwezo wa Mwenyezi Mungu na kupigana vita dhidi ya wajumbe Wake.

Nabii Musa (AS) alionyesha njia kwa watu na akatufundisha ni watu gani tunapaswa kuwakataa na kujiepusha nao.

captcha