IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Musa/16

Musa Alitumia Dua katika Njia ya Utume

18:35 - July 25, 2023
Habari ID: 3477337
TEHRAN (IQNA) – Katika historia, tangu Mtume wa kwanza wa Mwenyezi Mungu alipokanyaga ardhini, hakuna mtu ambaye ameweza kuwaelimisha watu katika ngazi ya mtu binafsi na ya kijamii bora kuliko Mitume na Maimamu watoharifu wa nyumba ya Mtume Muhammad (SAW).

Kwa hiyo ni muhimu kujifunza mbinu za kuelimisha walizotumia. Moja ya njia hizi ni kutumia dua. Dua ni ombi la unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, ambaye hana haja kabisa. Dua na maombi yapo kwa namna tofauti katika mataifa na dini zote.

Jambo muhimu zaidi kuhusu dua ni kwamba ni tangazo la haja na kumtegemea Mwenyezi Mungu, Muumba wa Mbingu na Ardhi.

Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu, Mwenyewe, amewaamuru wanadamu kusali na kusoma dua.

Musa (AS), ambaye alikuwa mjumbe mkuu wa Mwenyezi Mungu, alitumia njia ya maombi katika kuwaongoza watu. Hapa kuna mambo mawili kuhusu dua zake:

1- Adabu katika kuomba

Musa (AS) aliamua kwenda Midiani, iliyokuwa nje ya eneo lililotawaliwa na Firauni. Baada ya safari ndefu, alifika Midiani na kuwaona mabinti wa Nabii Shuaib (AS) pale. Alichota maji kisimani kwa ajili ya wasichana na kuwanywesha mifugo yao. Akiwa na njaa na uchovu, alijilaza chini ya kivuli cha mti na akaomba: “Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia.  Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema: Baba yangu anakwita akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipo mjia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwisha okoka kwenye watu madhaalimu." Aya za 24 na 25 zaa Sura Al-Qasas).

Ingawa alikuwa amechoka na mwenye njaa, hakujua mtu yeyote katika jiji hilo na hakuwa na kimbilio, hakutenda bila subira bali alizungumza tu juu ya yale aliyohitaji na kungojea kibali cha Mungu.

2- Dua kabla ya kuanza utume

Musa (AS) alipojifunza kuhusu umuhimu wa utume wake, alimwomba Mungu na kuomba mambo machache ili kuweza kutimiza utume wake vizuri.

Moja ya mambo aliyoomba ni "kupanuka kifua".

“(Musa) akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nikunjulie kifua changu,”. (Aya ya 25 ya Surah Taha)

Kwa kuomba upanuzi wa kifua chake, alikuwa anamwomba Mwenyezi Mungu ajaze moyo wake kwa ujasiri ambao unaweza kumwezesha kutekeleza majukumu yanayohusiana na utume mkuu wa mjumbe, na kumpa uvumilivu, uthabiti na ustahimilivu.

Hivyo mtu anaweza kujifunza mafunzo kutokana na nukta hizi mbili katika dua za Musa (AS).

Kwanza, ni muhimu kwamba mtu anapaswa kumwomba Mwenyezi Mungu mambo anayotaka kwa unyenyekevu na hapaswi kutenda kana kwamba Mwenyezi Mungu ana deni kwake.

Jambo lingine ni kwamba mtu anapaswa kujua kwamba kabla ya kuanza utume wowote ule, anapaswa kujiandaa kiakili na kiroho na kufika katika hali ya juu kabisa ya utayari wa kazi hiyo, ikiwa ni pamoja na kumuomba Mungu ampe utayari wa kiwango hicho.

captcha