IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Nuhu/36

Umuhimu wa Kuendelea katika Elimu

16:46 - November 22, 2023
Habari ID: 3477927
TEHRAN (IQNA) – Kama ilivyo katika nyanja nyingine nyingi, kudumisha uendelevu na uthabiti ni muhimu sana kwa mafanikio katika nyanja ya elimu.

Kuwa na mwendelezo ni miongoni mwa sifa za kawaida za watu wote waliofanikiwa. Njia mojawapo ya mbinu za elimu ni ile ya kuendelea na Mitume wa Mwenyezi Mungu waliitumia kwa vile wamekuja kuwaongoza na kuwaelimisha wanadamu na hivyo Tabshir zao (kutoa habari njema) na Inza (maonyo) ziwe zenye kuendelea na zisizokatika.

Ikiwa mwaliko wa mema ni wa muda mfupi, watu hawatautilia maanani ipasavyo.

Nabii Nuhu au Nuh (AS) alilipa umuhimu maalum suala la kuendelea kutekeleza wajibu wake kama mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa aya za Qur'ani Tukufu, alikuwa imara katika juhudi zake za kuwaongoza watu wake kwenye njia iliyonyooka.

Tunasoma katika Aya za 5-9 za Surah Nuh ndani ya Quran Tukufu:

“Akasema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimewaita watu wangu usiku na mchana,  Lakini wito wangu haukuwazidisha ila kukimbia.  Na hakika mimi kila nilipo waita ili upate kuwaghufiria, walijiziba masikio yao kwa vidole vyao, na wakajigubika nguo zao, na wakakamia, na wakatakabari vikubwa mno!  Tena niliwaita kwa uwazi. Kisha nikawatangazia kwa kelele, tena nikasema nao kwa siri."

Aya hizi zinabainisha uimara wa Nuhu na kuendelea katika kuwaelimisha watu, kuwalingania kwenye njia iliyonyooka na dini ya Mwenyezi Mungu mchana na usiku na faraghani na hadharani.

captcha