IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Maadui wanataka kuvuruga uhusiano wa Iran na majirani zake

18:02 - May 20, 2023
Habari ID: 3477024
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amegusia mpaka mrefu uliopo baina ya Iran na majirani zake kadhaa na kusema kuwa, maadui wameazimia kuzusha matatizo katika uhusiano wa Tehran na majirani zake, hivyo lazima tuwe macho na tusiruhusu kufanikiwa siasa zao hizo

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo Jumamosi wakati alipoonana na viongozi na maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na mabalozi wa Jamhuri ya Kiislamu nje ya Iran na kusisitiza kuwa, siasa za kuwa na mawasiliano mazuri na nchi za Kiislamu hata zilizoko mbali na Iran ni muhimu sana. Pia amesema, siasa za kuwa na mawasiliano na nchi zenye muelekeo sawa na Iran, aidha ni jambo muhimu sana. 

Amesema, leo hii ushirikiano wa karibu wa Iran na nchi kubwa na zenye siasa zinazofanana na Jamhuri ya Kisilamu katika masuala tofauti ya kimsingi kwenye siasa za kimataifa umeongezeka sana na inabidi fursa hii tuitumie vizuri katika kuimarisha na kutia nguvu mawasiliano na ushirikiano wetu na nchi hizo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amebainisha pia vielelezo vinavyozingatiwa katika siasa za kigeni zenye mafanikio akisema: Kwanza ni "heshima" kwa maana ya kujiweka mbali na diplomasia ya kubembeleza, pili ni "hikma" kwa maana ya kuamiliana na wengine kwa busara na mahesabu mazuri na tatu ni "maslahi" kwa maana ya kukubali kulegeza baadhi ya misimamo kwa ajili ya kuepuka vizingiti na vizuizi vigumu na kuendelea mbele na harakati zako.

Amesisitiza kuwa, hiyo ni misingi mitatu mikuu na muhimu sana katika diplomasia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Ayatullah Khamenei amesema pia kuwa, kutoziamini kibubusa pande nyingine ni upande mwingine wa maana ya hikma na kusisitiza kwa kusema: Tab'an hatupaswi kuchukulia kila neno linalosemwa duniani kuwa ni uongo kwani yako pia maneno ya kweli na yanayokubalika, lakini pia hatupaswi kuamini kila linalosemwa.

4141898

Habari zinazohusiana
captcha