IQNA

Kadhia ya Palestina

Ayatullah Khamenei: Vita vya Gaza vimefichua 'Uso Mbaya' wa Uingereza, Marekani

23:46 - December 23, 2023
Habari ID: 3478081
IQNA-Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema utawala wa Israel hauwezi kufanya jinai nyingi kiasi hiki dhidi ya Wapalestina huko Ghaza bila ya uungaji mkono wa Marekani na Uingereza.

Akizungumza katika mkutano wa Jumamosi mjini Tehran na umati wa watu kutoka mikoa wa Kerman na Khuzestan, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei alisema kura ya turufu ya Marekani dhidi ya maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kusimamisha vita na kusitishwa kwa mashambulizi ya mabomu huko Gaza ni "kitendo kisicho na aibu" na "ni ushirikiano na utawala wa Kizayuni katika kudondosha  mabomu yanayowalenga watoto, wanawake, wazee, wagonjwa na watu wengine wasio na ulinzi".

"Ushindi mkubwa wa taifa la Palestina na Mrengo Mtakatifu wa Muqawama (Mapambano ya Kiislamu) ni kwamba umeweza kuvunja itibari ya madola ya Ulaya na Marekani na kufichua asili ya madai yao yote ya uwongo ya haki za binadamu, kwani Israel haikuweza kufanya jinai nyingi bila ya msaada wa Marekani.

"Na leo hii sura mbaya ya wanyama wakali wa kutisha yaani Marekani na Uingereza imefichuliwa kwa watu wote wa dunia, na asili ya Ikulu ya Marekani imefichuliwa na dhatu ya ndani ya serikali za Marekani na Uingereza umefichuliwa," Press TV ilimnukuu akisema.

Msaada wa Mwenyezi Mungu

"Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, mrengo wa  haki bila shaka utashinda na utawala ghasibu wa Kizayuni utatokomezwa, na tunatumai nyinyi, vijana, mtauona mustakbali huu kwa macho yenu wenyewe," alisema.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia kadhia ya kimataifa na Kiislamu ya Gaza na kusema: Tukio hili ni la kipekee katika nyanja mbili; kwa upande si la kawaida kwa utawala wa Kizayuni, kwa sababu ukatili huu, jinai, umwagaji damu, mauaji ya watoto wachanga, uovu, ukatili, na kurusha mabomu juu ya vichwa vya wagonjwa na hospitali ni mambo ambayo hayakuwahi kushuhudiwa; na kwa upande wa wananchi wa Palestina na wanamapambano wa Kipalestina halina mithili kwa sababu subira kama hii, kusimama kidete namna hii na kumfanya adui awe mwendawazimu ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri

Ayatullah Khamenei amebainisha: Ingawa maji, chakula, dawa na mafuta hayawafikii watu hawa, lakini wao wamesimama kama mlima, na kutosalimu amri kutawafanya washinde kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri, kama ambavyo tayari ishara za ushindi zimeanza kuonekana.

"Kutokukata tamaa kunawafanya kuwa washindi, ingawa dalili za ushindi zinaweza kuonekana leo," Ayatullah Khamenei aliongeza, akinukuu Quran Tukufu inayosema "Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na wanaosubiri."

Utawala wa Israel, Kiongozi Muadhamu amesema, "ukiwa na zana zote na suhula zote, bado hauna nguvu dhidi ya wapiganaji wa Kipalestina, ambao zana zao haziwezi kulinganishwa na zana za utawala wa Kizayuni".

"Kufeli utawala wa Kizayuni katika tukio hili pia ni kushindwa kwa Marekani, na leo hii hakuna mtu yeyote duniani anayetofautisha kati ya utawala ghasibu (wa Israel) na Marekani na Uingereza, na kila mtu anajua kuwa wao ni kitu kimoja."

Kususia Israel

Kiongozi Muadhamu alisema serikali na mataifa yana wajibu wa kusaidia wanamuqawama au wapigania ukombozi wa Palestina kwa njia yoyote ile inayowezekana. "Kusaidia muqawama ni jukumu la kila mtu, na kuusaidia utawala wa Kizayuni ni uhalifu na uhaini," alisema.

Ayatullah Khamenei alionyesha masikitiko yake juu ya usaidizi wa "kihalifu" wa baadhi ya mataifa ya Kiislamu kwa utawala wa Kizayuni, akisema mataifa ya Kiislamu hayatasahau nukta hiyo.

Serikali za Kiislamu, alisema, "zina jukumu la kuzuia utawala wa Kizayuni usipate bidhaa, mafuta na nishati kwani utawala huo umezuia hata maji kuwafikia watu wa Gaza".

"Mataifa ya Kiislamu yanapaswa kuziomba serikali zao kukata uhusiano na misaada yoyote kwa wahalifu wa Kizayuni, au ikiwa hawawezi kukata uhusiano wa kudumu, angalau kuweka shinikizo kwa utawala mbovu, katili na wa umwagaji damu kwa kuwakatisha kwa muda."

Leo, Kiongozi Muadhamu alisema, dhamiri za ulimwengu zimeumizwa kutokana na unyama wa Israel.

"Watu wa Marekani na Ulaya wanaingia mitaani na baadhi ya viongozi wa kisiasa na marais na wanasayansi wao wa vyuo vikuu wanapinga uungaji mkono wa serikali zao kwa utawala wa Kizayuni, lakini pamoja na hayo, baadhi ya serikali zinaendelea kuusaidia utawala huo katili."

Habari zinazohusiana
captcha