IQNA

Kadhia ya Palestina

Ayatullah Khamenei apanda mzeituni katika mshikamano na Wapalestina

19:53 - March 05, 2024
Habari ID: 3478453
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepanda mzeituni katika hatua ambayo ameitaja kuwa ni mshikamano na wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu leo ​​(Jumanne) baada ya kupanda miche mitatu kwa mnasaba wa Siku ya Upandaji Miti Iran aameashiria kuhusu namna Uislamu unavyolipatia umuhimu suala la uhusiano kati ya mwanadamu na mazingira na pia utunzaji wa mazingira, ambapo amepanda miche mitatu ukiwemo mzeituni ili kuonyesha umakini zaidi katika upandaji miti na kuongeza kuwa: "Mwaka huu tumepanda miche mitatu ili kuonyesha umakini zaidi katika upandaji miti. Kati ya miche hii mitatu ni mzeituni kwa ajili ya kutangaza mshikamano na huruma kwa watu wanaodhulumiwa wa Palestina ambao ardhi yao ni kitovu cha mizeituni. Tunataka kuwatumia salamu za mbali watu hawa azizi na wenye uwezo mkubwa wa mapambano na tunawafahamisha kuwa tunawakumbuka kwa njia zote na njia mojawapo ni kwa kupanda mzeituni."

Ayatullah Khamenei aidha ameashiria Siku ya Upandaji Miti Iran na kutaja upandaji miti kuwa ni uwekezaji wa gharama nafuu na wenye faida na kuongeza kuwa: "Mti una matunda mengi kama vile kuongeza hewa ya oksijeni na kupambana na uchafuzi wa mazingira, hivyo ni uwekezaji wenye faida hasa katika maisha ya kimashine ya leo." Aidha amesema, kwa bahati mbaya, uchafuzi umeongezeka.

Mbali na kupanda mzeituni, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu pia amepanda mche mmoja wa mteashuri na mwingine wa mtini ambao ulizalishwa nchini.
Mtini ni mti wa asili wa misitu ya Mazandaran, ambao pamoja na kutumika mbao zake ngumu kwa malengo mbalimbali, mizizi na majani yake pia hutumika kwa ajili ya dawa.
Nchini Iran, Machi 5 hadi 12 inaitwa "Wiki ya Maliasili" ambapo siku ya kwanza ya wiki hii (Machi 5) ni siku ya upandaji miti.

 
 

4203635

 

Habari zinazohusiana
captcha