IQNA

Kadhia ya Palestina

Kiongozi Muadhamu atoa wito kwa nchi za Kiislamu kukata mishipa ya uhai wa utawala wa Kizayuni

16:32 - January 23, 2024
Habari ID: 3478242
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa: Nchi za Kiislamu zinapaswa kukata uhusiano wao wa kisiasa na kiuchumi na utawala wa Kizayuni kwa kukata mishipa muhimu ya uhai ya utawala huo ghasibu.

Kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Ofisi ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu akizungumza leo jijini Tehran katika kikao na waandaaji wa Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Mashahidi 22,000 kutoka Mkoa wa Tehran, amekosoa utendaji wa viongozi wa nchi za Kiislamu kuhusiana na suala muhimu sana la Gaza na kusema: Wakati fulani misimamo na matamshi ya viongozi hao nchi za Kiislamu ni makosa kwa sababu wanazungumzia suala kama vile usitishaji vita huko Gaza, ambalo liko nje ya uwezo wao na liko chini ya udhibiti wa adui muovu wa Kizayuni.
Ayatullah Khamenei ameongeza kuwa: Licha ya utendaji usiofaa wa maafisa wa nchi za Kiislamu na licha ya matatizo yote yaliyomo, tunasoma katika Qur'ani Tukufu kwamba Mwenyezi Mungu yuko pamoja na watu waaminifu na popote pale alipo Mwenyezi Mungu kutakuwa na ushindi.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameongeza kuwa: Ushindi wa watu wa Gaza ni wa uhakika, na Mwenyezi Mungu Mtukufu atauonyesha ushindi huo Umma wa Kiislamu katika mustakabali usio mbali, na nyoyo za Waislamu hususan watu wa Palestina na Gaza watakuwa na furaha.

4195479

 

 

 

Habari zinazohusiana
captcha