IQNA

Taazia

Kiongozi Muadhamu aongoza Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Shahidi Mousavi

20:48 - December 28, 2023
Habari ID: 3478105
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, leo asubuhi ameongoza Sala ya Maiti ya kuusalia mwili wa Kamanda Shahidi Sayyid Razi Mousavi pamoja na kumsomea Faatiha na kumuombea dua Shahidi huyo.

 

Aidha, Ayatullah Khamenei ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya Shahidi Sayyid Razi Mousavi na akatoa shukurani na kuienzi Jihadi aliyopigana bila kuchoka Shahidi huyo; na akamuombea dua ya kupandishwa daraja yake na Allah na kuwa pamoja na mawasii na mawalii wa Mwenyezi Mungu.

Kamanda Sayyid Razi Mousavi, mmoja wa washauri wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), ambaye alikuwa akishughulikia masuala ya kilojistiki katika kuunga mkono Mhimili wa Muqawama nchini Syria, aliuawa shahidi siku ya Jumatatu katika shambulio la kigaidi lililofanywa na utawala wa Kizayuni kwenye eneo la Zainabiyah katika mji mkuu Damascus.

Shahidi Razi Mousavi alikuwa mmoja wa washauri wa muda mrefu wa Kikosi cha Quds cha IRGC nchini Syria na msaidizi na mtu wa karibu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani.

Kabla ya kusafirishwa kuletwa hapa nchini, mwili wa Shahidi Sayyid Razi Mousavi jana Jumatano ulisindikizwa na hadhara ya maelfu ya wananchi wa Iraq na wapiganaji wa Muqawama wa Kiislamu wa nchi hiyo katika mji wa Najaful-Ashraf na kufanyiwa tawafu katika Haram tukufu ya Imam Ali (AS).

Sayyid Mojtabi al-Hussaini, mwakilishi wa Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu huko Najaful-Ashraf, aliongoza Sala ya Maiti uliyosaliwa mwili wa Shahidi Mousavi katika mji huo. Kabla ya hapo pia, shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Shahidi Mousavi ilifanyika katika Haram za Bibi Zainab na Bibi Ruqayyah (AS) nchini Syria.

Hapa mjini Tehran, shughuli ya kuusindikiza na kuuaga mwili wa Shahidi Mousavi imefanyika leo katika uwanja wa kidini wa Imam Hussein (AS) na maziko yake yanafanyika kwenye kitongoji cha Tajrish katika eneo la Imamzadeh Saleh (AS).

4190403

Habari zinazohusiana
captcha