IQNA

Teknolojia katika Uislamu

Programu ya Kidijitali Iliyoundwa Pakistani Inahakikisha uchapishaji Qur'ani Tukufu bila hitilafu

8:04 - August 28, 2023
Habari ID: 3477507
ISLAMABAD (IQNA) – Msomi mmoja wa Pakistani ametengeneza programu ya kidijitali ya Qur'ani Tukufu ambayo hurahisisha kupata na kusoma Qur'ani Tukufu. Programu hiyo aidha inahakikisha kuwa uchapishaji Qur'ani Tukufu unafanyika bila makosa.

Kuna watu wengi ambao wamejitolea maisha yao kwa ajili ya kazi ya Qur'ani Tukufu na mafundisho ya Qur'ani Tukufu na baadhi yao wameacha alama zao zisizoweza kufutika katika historia kuhusiana na suala hili.

Hassan Rashid Ramey ni mmoja wa watu kama hao ambaye amefanikiwa kuunda programu ya kidijitali ya Qur'ani Tukufu

Hassan Rashid Ramey, mwanae marehemu Rashid Ahmad Chaudhry, kaka wa mwanasiasa maarufu, mchoraji, mhariri, na msomi Muhammad Hanif Ramey, alijitolea zaidi ya miaka 20 ya maisha yake kutengeneza programu hii ili kufanya ufikiaji na kusoma Qur'ani Tukufu kuwa rahisi na kupatikana zaidi.

Programu ya kidijitali iliyotengenezwa na Hassan Rashid Ramey sasa inajivunia zaidi ya watumizi milioni moja.

Wakati wa mazungumzo yasiyo rasmi na Pakistan Today, Hassan Rashid Ramey alibainisha mawazo yake kuhusu safari ya ajabu ya jitihada hii ya kuthibitisha imani, ambayo inajumuisha Qur'ani Tukufu, vitabu, programu, teknolojia ya habari, na huduma zinazohusiana na Qur'ani Tukufu.

Alisema ujio wa enzi ya dijitali umeleta mageuzi katika usambazaji wa mafundisho ya kidini, na teknolojia ya kompyuta imekuwa na jukumu muhimu. Qur'ani Tukufu sasa inapatikana kwa urahisi katika muundo wa kidijitali, na ni muhimu kuimarisha maendeleo ya haraka ya teknolojia ya habari kwa ajili ya huduma ya mafundisho ya Qur'ani, alisema.

Ramey alidokeza kwamba programu hii inahakikisha uhifadhi sahihi wa kila herufi katika Qur'ani Tukufu, na kuondoa uwezekano wa makosa ambayo yanaweza kutokea wakati wa kisomo. "Pia inahakikisha uadilifu wa maandishi na kuzuia upotoshaji. Programu hiyo hurahisisha uchapishaji mzuri wa Qur'ani Tukufu mchakato ambao ulikuwa ukichukua miaka kadhaa kwa waandishi wenye ujuzi kuukamilisha”, alisisitiza.

3484947

Habari zinazohusiana
captcha