IQNA

Washindi wa Mashindano ya Nane ya Qur'ani Ulaya wazawadiwa

14:37 - May 02, 2022
Habari ID: 3475195
TEHRAN (IQNA)- Sherehe za kufunga Mashindano ya Nane ya Qur'ani Barani Ulaya zimefanyika wikiendi hii.

Washindi wametunukiwa zawadi katika mahafali iliyofanyika katika Kituo cha Kiislamu cha Hamburg. Majaji walimtangaza Ali Bayt kuwa mshindi katika kategoria ya qiraa ya wanaume huku nafasi za pili na tatu zikishikiliwa na Mostafa Ahmadian na Mojtaba Mahmoud.

Abbas Sharifi na Amin Taqi wameshika nafasi ya kwanza katika  Adhana na qiraa.

Mashindano hayo yameandaliwa na taasisi ya Darul Quran ya Ujerumani ambayo inafungamana na Kituo cha Kiislamu cha Hamburg katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu kutoka madhehebu zote za Kiislamu wanaoishi Ulaya  walikuwa na uwezo wa kujisajili katika mashindano hayo ambayo yalikuwa na makundi ya chini ya miaka 16 na juu ya miaka 16.

Lengo la mashindano hayo ya kia mwaka limetajwa kuwa ni kustawisha utamaduni wa Qur'ani na kutambua na kukuza vipawa vya Qur'ani barani Ulaya.

 

Winners of 8th European Quran Contest Awarded

Winners of 8th European Quran Contest Awarded

Winners of 8th European Quran Contest Awarded

 

4054352

4054352

 

Habari zinazohusiana
Kishikizo: qurani tukufu
captcha