IQNA

Qur'ani Tukufu

Tahadhari kuhusu nakala za Qur’ani Tukufu zilizopotoshwa katika intaneti

21:51 - December 09, 2022
Habari ID: 3476222
TEHRAN (IQNA) – Waislamu wametakiwa kuchukua tahadhari kuhusu nakala za Qur’ani Tukufu zilizo katika mitandao ya intaneti na aplikesheni kwani imebainika kuwa baadhi zimepotoshwa kwa makusudi.

Jumuiya ya Kiislamu Duniani imetoa taarifa na kutangaza kuwepo nakala za Qur’ani Tukufu zenye makosa na potofu kwenye baadhi ya tovuti zisizojulikana na kusema kwamba wanazuoni wa Kiislamu wanapaswa kuwa na msimamo kuhusu suala hili.

Taarifa hiyo imesema: “Kuna nakala potofu ya Qur'ani Tukufu kwenye baadhi ya tovuti, ambazo zina makosa na pia zingine zina nyongeza katika baadhi ya maandiko yake.

Jumuiya ya Kiislamu Duniani iliwataka Waislamu wote pamoja na viongozi wa Kiislamu kote ulimwenguni kuchukua tahadhari kuhusu ya matumizi ya tovuti zisizojulikana na nakala potofu za Qur’ani Tukufu kwenye mitandao.

Jumuiya hii ilisema: Tunaomba kila mtu ashikamane na tovuti ambazo zinazojulikana na nakala sahihi ya Qur’aniTukufu.

Jumuiya ya Kiislamu Duniani iliwataka wasomi na wahubiri wa Kiislamu kuwa makini na  kuwafahamisha watu wote kuhusu suala hili na kuwataka wawe na tahadhari katika kutumia nakala za Qur'ani Tukufu zilizo katika mitandao.

/4105629

captcha