IQNA

Shughuli za Qur'ani Misri

Al-Azhar kuimarisha vituo vya Qur'ani Tukufu kwa watoto

21:57 - December 20, 2022
Habari ID: 3476277
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri kimetangaza kuwa vituo 538 vya watoto vimezinduliwa hivi karibuni.

Al-Azhar imezindua vituo 538 vya masomo ya Qur'ani Tukufu kwa ajili ya watoto katika vijiji na maeneo ya mbali ya nchi hiyo ya Kiarabu, na kufanya jumla ya vituo hivyo kufikia 1045.

Watoto wanaovutiwa na kozi za Qur'ani Tukufu za kusoma au kuhifadhi wanaweza kufanya mtihani wa kuingia na kuanza kujifunza kwenye vituo hivyo.

Sheikh Abdelmuneim Fuad, Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar , anasema mipango inaendelea kutatua matatizo ya vituo hivyo na kuvipa teknolojia mpya.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

Shughuli za Qur'ani hufanyika kwa wingi sana Misri ambapo wasomaji maarufu zaidi wa Qur'ani  Tukufu duniani ni kutoka Misri.

4108377

Habari zinazohusiana
captcha