IQNA

Mtazamo

Sheikh Mkuu wa Al Azhar: Binadamu Anahitaji Mwongozo wa Qur'ani Tukufu

16:01 - April 07, 2024
Habari ID: 3478645
IQNA - Imamu mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri alisema matukio machungu yanayotokea duniani yanadhihirisha ukweli kwamba ubinadamu unahitaji mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

Sheikh Ahmed al-Tayyeb alisema ubinadamu haujawahi kuhitaji zaidi mwongozo wa Qur'an kama ilivyo hivi sasa, al-Watan iliripoti.

Alikuwa akizungumza katika hafla iliyofanyika Jumamosi usiku katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa al-Manara mjini Cairo kwa mnasaba wa Usiku wa Qadr. Sheikh al-Tayyeb alionya kwamba ulimwengu umepoteza uongozi wa busara na unaelekea katika maporomoko kama wakati mwingine wowote katika historia.

Baada ya miongo kadhaa ya mazungumzo ya kistaarabu kati ya mataifa, mazungumzo sasa yamebadilishwa na mivutano na migongano kwa njia ya kushangaza, amebaini kwa masikitiko.

Mkuu huyo wa Al-Azhar ameongeza kuwa walio nyuma ya mapigano na vita hivi ni viongozi wa kisiasa na kijeshi wenye mioyo ya mawe mbali na huruma ya Mwenyezi Mungu.

Akiashiria vita vya utawala wa Israel dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, amesema wanajeshi wa Israel wanakabiliana na raia na watu wasio na ulinzi ambao hawajui chochote kuhusu vita au mauaji.

Kuna watoto wasio na ulinzi, wanawake na wagonjwa (huko Gaza) ambao miili yao imeachwa mitaani au kusalia chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa, alisema.

Vita vya utawala wa Israel dhidi ya Gaza vilivyoanza tarehe 7 Oktoba 2023 vimesababisha vifo vya zaidi ya Wapalestina 33,000 wengi wao wakiwa wanawake na watoto na wengine wengi kujeruhiwa.

3487841

Kishikizo: al azhar gaza tayyeb
captcha