IQNA

Harakati za Qur'ani

Binti wa Kimisri aliyehifadhi Qur'ani Tukufu na Hadithi 6000 aenziwa na Al-Azhar

20:26 - May 23, 2023
Habari ID: 3477034
TEHRAN (IQNA) – Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri kilimtunuku msichana barobaro ambaye amehifadhi Qur’ani Tukufu kikamilifu na Hadith 6,000 za Mtume Muhammad SAW pamoja na mashairi ya Kiarabu.

Fatimah al-Bandari, ambaye aliwakilisha Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar katika shindano la hivi majuzi la kusoma nchini kote, alishika nafasi ya kwanza katika shindano hilo, tovuti ya Cairo24 iliripoti.

Pia hapo awali amekuwa wa kwanza katika mashindano ya kusoma na Al-Azhar ili kuhimiza kizazi kipya kusoma vitabu vya Kiislamu na kudumisha turathi na utamaduni wa Kiislamu.

Hapo awali, Fatimah alikuwa ametwaa tuzo ya juu zaidi katika shindano la usomaji wa vitabu la Ulimwengu wa Kiarabu lililofanyika Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.

Alisema katika mahojiano ya hivi majuzi ya runinga kwamba alianza kuhifadhi Qur'ani Tukufu akiwa na umri wa miaka 3 na akafanikiwa kuhifadhi Kitabu hicho kitakatifu kwa moyo kikamilifu mwaka mmoja baadaye. Kwa sasa Fatimah ni mwanafunzi katika shule ya upili inayohusishwa na Chuo cha Kiislamu cha Al-Azhar.

3483664

Kishikizo: al azhar qurani tukufu
captcha