IQNA

Kimbunga cha Al Aqsa

Shekhe Mkuu wa Al-Azhar apongeza ushujaa wa watu wasio na ulinzi wa Gaza

19:35 - October 31, 2023
Habari ID: 3477821
CAIRO (IQNA) – Sheikhe mkuu wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amesifu ushujaa na ujasiri wa watu wa Ukanda wa Gaza katika kukabiliana na mashambulizi makali ya Israel.

Katika ujumbe siku ya Jumatatu, Sheikh Ahmed al-Tayeb alituma salamu kwa watu "mashujaa" wa Gaza ambao wanastahimili ndege za kivita, meli za kivita, na makombora ya adui kwa imani yao.

Alitoa wito kwa Wapalestina wa Gaza kupata ilhamu na motisha kutoka kwa Qur’ani Tukufu, akinukuu Aya ya 139 ya Surah Al Imran: “Wala msilegee, wala msihuzunike, kwani nyinyi ndio wa juu mkiwa ni Waumini.”

Aidha amelaani ukatili unaofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel katika mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya nyumba, misikiti, makanisa, hospitali na shule katika Ukanda wa Gaza na kuwaua wanawake, watoto, waandishi wa habari na raia wengine wasio na hatia.

Sheikh al-Tayeb pia alipongeza misimamo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika kutoa wito wa kukomeshwa uvamizi wa Israel dhidi ya Gaza.

Alitoa wito kwa watu wote mashuhuri duniani kutonyamaza bali kulaani mauaji ya kinyama ya watu huko Gaza.

Aidha amezitaka serikali za nchi za Kiarabu na Kiislamu kuwasaidia wenzao huko Palestina katika kukabiliana jinai za Israel.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya katika Ukanda wa Gaza, hadi kufikia jioni ya leo idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo inakaribi watu 9,000, wakiwemo watoto zaidi ya 3,500.

3485811

Habari zinazohusiana
captcha