IQNA

Mashindano ya Qur'ani

Mashindano ya Al-Azhar kubainisha vipaji vya Qur’ani

7:34 - October 18, 2022
Habari ID: 3475948
TEHRAN (IQNA) - Shirika la shule za Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar nchini Misri limetangaza kuanza kwa mchakato wa usajili kwa wale walio tayari kushiriki katika mashindano ya kila mwaka ya Qur’ani ya kituo hicho.

Idara ya Masuala ya Qur'ani ya Al-Azhar kila mwaka huandaa mashindano hayo kati ya wanafunzi wa shule zilizounganishwa na kituo hicho kote Misri chini ya usimamizi wa mkuu wa Al-Azhar Sheikh Ahmed el-Tayyeb.

Ilisema tukio la mwaka huu la Qur'ani litafanyika katika ngazi nne za kuhifadhi Qur'ani, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi Qur'ani nzima kwa Tarteel na kuhifadhi Juzuu 20 za Qur’ani Tukufu

Waombaji wanapaswa kuwa wanafunzi wa shule zinazoshirikiana na Al-Azhar na vituo vya kuhifadhi Qur'ani na wawe na umri wa chini ya miaka 18.

Washindi watatunukiwa zawadi za pesa taslimu kuanzia pauni 22,000 hadi 100,000 za Misri, waandaaji wanasema.

Misri ni nchi ya Afrika Kaskazini yenye wakazi wapatao milioni 100. Waislamu ni takriban asilimia 90 ya watu wote wa nchi hiyo.

4092384

captcha