IQNA

Jinai za Israel

Israel imeua zaidi ya wahubiri 100 na kubomoa misikiti 1,000 katika vita vya mauaji ya kimbari Gaza

19:27 - January 22, 2024
Habari ID: 3478234
IQNA-Wizara ya Wakfu na Masuala ya Dini katika Ukanda wa Gaza imesema mashambulizi ya vikosi vya utawala katili wa Israel dhidi ya eneo hilo lililozingirwa yamebomoa na kuharibu misikiti 1,000 tokea Oktoba 7 mwaka uliopita hadi sasa.

Aidha zaidi ya wahubiri 100 wa Kiislamu pia wameuawa katika hujuma mbaya ya Israel dhidi ya Gaza, Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kidini ilisema katika taarifa yake Jumapili, na kuongeza kuwa kanisa, majengo kadhaa ya utawala na shule za Qur'ani zimeharibiwa katika vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya eneo hilo la pwani.

Kati ya misikiti iliyobomolewa kwa makombora ya Israel ni Msikiti Mkuu wa Omari, mojawapo ya misikiti muhimu na ya kale katika Palestina  na pia utawala huo wa Kizayuni umelenga makanisa machache yaliyoko Gaza. Jeshi la Israel limelenga kwa mabomu Kanisa la Mtakatifu Porphyrius, linalofikiriwa kuwa kanisa la tatu kwa kongwe duniani kote.
"Ujenzi mpya wa misikiti hii utagharimu karibu dola milioni 500," ilisema taarifa hiyo.
"Utawala vamizi Israel unaendelea kuharibu makumi ya makaburi na kuchimba makaburi, kukiuka utakatifu wao ... na kuiba maiti ndani, katika changamoto ya wazi kwa mikataba ya kimataifa na haki za binadamu," ilisema.
"Tunatoa wito kwa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu na watu wenye dhamiri kutekeleza majukumu yao kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza," iliongeza.

Kadhalika hujuma hizo za Israel dhidi ya Gaza zimeripotiwa kulenga ofisi za kamati za kukusanya zaka, madrasa za Qurani na makao makuu ya Benki ya Wakfu.

Hii ni katika hali ambayo, shirika huru la kutetea haki za binadamu la Euro-Med Human Rights Monitor limeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umewauwa shahidi maprofesa 94 wa vyuo vikuu, mamia ya walimu, na maelfu ya wanafunzi katika Ukanda wa Gaza katika muda wa miezi mitatu iliyopita.


Utawala wa Kizayuni ilianzisha kampeni ya kijeshi dhidi ya Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 7, na hadi kufikia tarehe 22 Januari utawala huo katili ulikuwa umeua zaidi ya Wapalestina  25,000 - wengi wao wakiwa wanawake na watoto - na kujeruhi takriban 62,000.
Mashambulizi ya Israel yamewafanya zaidi ya asilimia 85 ya wakazi wa Gaza kuyahama makazi yao na kutekeleza mzingiro wa jumla na kusababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.
Pia imeharibu angalau asilimia 60 ya miundombinu ya eneo hilo kupitia kulenga mara kwa mara hospitali, shule, vyuo vikuu na zaidi ya maeneo 100 ya urithi.
Hizi ni pamoja na makaburi ya Warumi yenye umri wa miaka 2,000 kaskazini mwa Gaza yaliyochimbwa tu mwaka jana, na Jumba la kumbukumbu la Rafah, eneo la kusini mwa Gaza ambalo lilijitolea kufundisha juu ya urithi wa eneo hilo refu na la tabaka nyingi - hadi lilipoharibiwa na mashambulio ya anga. mapema katika vita.

3486897

Habari zinazohusiana
captcha