IQNA

Jinai za Israel

Utawala wa Israeli umenyakua kinyume na sheria Msikiti, Kanisa, Sinagogi katika Ukingo wa Magharibi

16:38 - June 02, 2023
Habari ID: 3477080
TEHRAN (IQNA) – Utawala wa Israel umeripotiwa kuteka eneo la kihistoria la Wapalestina la Nebi Samuel, lililoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto unaoukalia kwa mabavu na makazi ya kanisa, msikiti na sinagogi, chini ya kisingizio "mbuga ya kitaifa".

Utekaji haramu wa Israel wa eneo hilo na kuwatiisha wakaazi wa asili wa Palestina ulifichuliwa na gazeti la Haaretz katika ripoti iliyofichua mojawapo ya njia nyingi ambazo utawala huo ghasibu unatekeleza maangamizi ya kikaumu ya  Waislamu asilia na jumuiya za Kikristo za Kipalestina kutoka katika Palestina ya kihistoria.

Kugeuza  miji na vijiji vya Wapalestina vilivyobomolewa kuwa ‘mbuga ‘wakati wa awamu ya kwanza ya mauaji ya umati yanayotekelezwa na Israel, ni mojawapo ya njia zenye mafanikio zaidi za ukoloni zinazotumiwa na utawala huo ghasibu. Wakati wa Nakba, yaani wakati wa kuundwa utawala haramu wa Israel, mwaka wa 1948 wakati zaidi ya Wapalestina 750,000-robo tatu ya wakazi wa asili wa Palestina walipotimuliwa katika ardhi zao - zaidi ya vijiji na miji 600 iliharibiwa kabisa. Maeneo mengi ya kulikojiri maangamizi ya umati ya Wapalestina yamegeuzwa kuwa mbuga.

Hatima kama hiyo inaonekana kuwangoja wakaazi wa Palestina wa Nebi Samuel. Eneo hilo linasemekana kuwa na kaburi la Nabii Samweli wa Biblia. Maelfu ya miaka ya historia imezikwa huko. Mahali hapa ni takatifu kwa Wayahudi, kwa Wakristo na kwa Waislamu. Kuna msikiti unaotumiwa kwa sala za  siku, na pembizoni mwa mlangoni mwake ni kanisa la Crusader.

Hadi Israel ilipokalia eneo hilo kwa mabavu mwaka 1967, msikiti na kaburi vilikuwa vimezungukwa na kijiji cha Nebi Samweli. Kijiji hicho kilikuwa na wakazi zaidi ya 1,000. Wengi wao walikimbia wakati wa Vita vya Siku Sita ambavyo Wapalestina wanaelezea kama mzunguko wa pili wa mauaji ya kikabila na Israeli. Wakaazi wa Kipalestina wa kijiji hicho walizuiwa kurejea makwao.

Mpango wa Israel wa kutwaa eneo hilo nyeti ulichukua sura madhubuti mwaka 1971 wakati waziri mkuu wa utawala huo Golda Meir alipowaamuru wanajeshi kubomoa nyumba 46 za kijiji hicho.

3483781

Habari zinazohusiana
captcha