IQNA

Uchambuzi kuhusu jinai za Israel

Familia za Palestina zaangamizwa na Israel, madola ya Magharibi yabakia kimya

22:29 - May 11, 2023
Habari ID: 3476989
TEHRAN (IQNA)- Katika mashambulizi yaliyofanywa juzi na utawala wa Kizayuni wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ambapo Wapalestina 15 waliuawa shahidi, zilichapishwa picha za uchungu huzuni za mwanamke na msichana mdogo wakiwaaga watu wa familia zao waliouliwa na jeshi la Israel, jambo ambalo limeumiza nyoyo na kuwatia watu simanzi na huzuni kubwa.

Katika jinai hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel, watu 3 wa familia moja yaani watoto wawili na baba yao, waliuawa shahidi. Msichana wa Kipalestina, Miral, pia alipoteza baba, mama na kaka yake katika hujuma hiyo ya kigaidi ya jeshi la Israel. Mwanamke wa Kipalestina ambaye mume na watoto wake wawili wameuwa kinyama na Israel alionekaka akimwaga machozi juu ya miili ya watoto wake wawili na mumewe, huku akishindwa kusimama wima. Msichana mdogo wa Kipalestina, Miral, pia anaonekana akilia katika video iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii na kupiga kelele: "Namtaka baba yangu." Miral alikuwa akimwita kwa uchungu baba yake, lakini ikabainika kuwa watu wote wa familia yake, yaani baba, mama na kaka yake wameuwa katika hujuma hiyo.

Watoto Wapalestina waachwa mayatima

Kuna watoto wengi kama Miral huko Palestina ambao walilala wakiwa pamoja na familia zao, lakini waliamka asubuhi wakiwa na maiti za jamaa, wazazi au ndugu zao. Walidhani wanaona ndoto, lakini ukatili na unyama wa utawala wa kigaidi wa Israel ulikuwa tayari umewatia siimanzi. Miral na watoto wengine mfano wake, watalazimika kuishi na machungu ya upweke na maumivu makali ya moyo na huzuni ya kupoteza wazazi wao.

ادامه درگیری‌ها در غزه و توقف تلاش‌ها برای آتش‌بس

Jambo linaloziidisha maumivu ni kwamba, picha za uchungu na maumivu za mwanamke huyo wa Kipalestina akiwaaga watoto na mumewe, na picha za kusikitisha zaidi za binti mdogo wa Kipalestina, Miral, akimlilia baba yake aliyekuwa amelala chini baada ya kuuliwa na wanajeshi wa Israel, ambazo zimechapishwa mara nyingi kwenye mitandao ya kijamii, zimepuuzwa kabisa katika ulimwengu unaoitwa uliostaarabu wa Magharibi. Picha hizo za kusikitisha na uhalifu wa utawala wa Kizayuni ambao ni mfano wa jinai dhidi ya ubinadamu, hazikuonyeshwa katika vyombo vya habari vya nchi za Magharibi wala kugusa nyoyo ziilizokufa za viongozi wa serikali zinazodai kutetea haki za binadamu za Magharibi.

Ubaguzi baina ya Palestina na Ukraine

Vyombo vya habari vya Magharibi na serikali za nchi hizo ziliandika na kutangaza mengi kadiri ilivyowezekana kuhusu mgogoro wa kibinadamu nchini Ukraine na kutangaza wasiwasi na huruma yao kuhusu suala hilo; lakini wanawake na wasichana wadogo wa Palestina hawana thamani yoyote mbele ya Wamagharibi kiasi kwamba hakuna hata haja ya kusikitishwa na mauaji yao! Huu ni mfano wa wazi wa mtazamo wa kibaguzi na kinafiki kuhusu haki za binadamu katika fikra na sera za nchi za Magharibi.

ادامه درگیری‌ها در غزه و توقف تلاش‌ها برای آتش‌بس

Waziri Mkuu, mawaziri wa serikali yake na maafisa wa kijeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanakiri rasmi kwamba hatua hiyo ni ya kigaidi na kusema kuwa, utawala huo umerejea katika sera za mauaji ya kigaidi dhidi ya wanamapambano wa Kipalestinai, lakini bado ulimwengu wa Magharibi uko kimya na umeamua kuziba macho na kutia pamba masikioni. Umoja wa Mataifa nao umeketi kando na kutazama kwa macho tu na hauchukui hatua yoyote angalau ya kuwaonea huruma akina mama na wasichana wadogo wa Kipalestina kama Miral.

Israel ni utawala wa kigaidi

Hapana shaka yoyote kwamba, Israel ni utawala wa kigaidi unaoua watoto; na nchi za Magharibi na Umoja wa Mataifa, kwa kimya chao ambacho kwa hakika si kimya bali ni uungaji mkono, ni washirika katika jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina. Himaya na uungaji mkono huu pia ni miongoni mwa sababu muhimu za kuendelea jinai za Wazayuni huko Palestina.

ادامه درگیری‌ها در غزه و توقف تلاش‌ها برای آتش‌بس

Kwa sababu hiiyo, Nasser Kan'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesisitiza kuwa: "Kunyamaza kimya na kutochukua hatua yoyote kwa jumuiya za kimataifa na nchi za Magharibi mbele ya ukatili unaoshadidi kila siku na hatua zilizodhidi ya binadamu za Wazayuni huko Palestina katika miezi ya hivi karibuni ndilo jambo muhimu zaidi linalozidisha kiburi cha utawala wa kibaguzi wa Israel katika kuendeleza jinai zake. Mwenendo huu utasajiliwa katika historia kama rekodi mbaya na ya kuaibisha, na kielelezo cha utendakazi mbovu wa wale wanaodai kuwa vinara wa kutetea haki za binadamu."

Habari zinazohusiana
captcha