IQNA

Jinai za Israel

Wapalestina 6 wauawa shahidi na jeshi la utawala dhalimu wa Israel huko Ukingo wa Magharibi

21:25 - October 25, 2022
Habari ID: 3475989
TEHRAN (IQNA)- Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshambulia makazi ya Wapalestina katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu, na kuua shahidi Wapalestina sita.

Jeshi hilo la Kizayuni limefanya mauaji hayo ya kikatili mapema leo Jumanne lilipovamia mji wa kale wa Nablus na vile vile mji wa Ramallah ulioko kaskazini mwa Palestina.

Inaarifiwa kuwa, Wapalestina wanne wameuawa shahidi katika mji wa Nablus, huku mmoja akiuawa shahidi katika eneo la Nabi Swaleh jijini Ramallah. Aidha Wapalestina zaidi ya 20 wamejeruhiwa vibaya kwenye hujuma hiyo ya Wazayuni maghasibu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Shehab, mmoja wa Wapalestina wanne waliouawa mjini Nablus ni alikuwa miongoni mwa viongozi wa harakati ya muqawama ya Arin al-Usuud (Pango la Simba), aliyefahamika kwa jina la Wadih al-Houh.

Zaher Jabareen, mwanachama wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama ya Palestina HAMAS sambamba na kulaani mauaji hayo amesisitiza kuwa: Tunawaomba watu wetu na makundi ya muqawama kusimama kidete dhidi ya ukaliaji wa mabavu (wa ardhi za Wapalestina).  

Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umeshadidisha mashambulizi yake dhidi ya Wapalestina huku ukipuuza sheria za kimataifa na haki za binadamu.

Hujuma na mashambulizi hayo hata hivyo yamejibiwa na makundi ya muqawama na wapigania uhuru wa Kipalestina hususan katika mji wa Nablus.

3480999

Habari zinazohusiana
captcha