IQNA

Mtazamo

Mwanazuoni wa Algeria aangazia mtazamo wa Imam Khomeini kuhusu hadhi ya wanawake

17:17 - February 09, 2024
Habari ID: 3478322
IQNA - Imam Khomeini (MA) alitilia mkazo hadhi ya juu ya wanawake katika Uislamu na alizingatia sana haki zao, mwanazuoni wa Algeria amesema.

Noura Farhat ameyasema hayo katika hotuba yake kwenye semina ya mtandaoni iliyofanyika kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 45 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Semina hiyo iliandaliwa Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA) siku ya Jumanne kwa jina la "Mwanamke wa Kuigwa wa Mapinduzi ya Kiislamu; Kujistahi na Kuhuisha Utambulisho wa Muislamu.”

Farhat amesema Imam Khomeini aliwaona wanawake kuwa moja ya nguzo za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kuendelea kwake.

Maoni yake juu ya wanawake yalitokana na mafundisho ya Kiislamu na hadhi ya Bibi Zahra (SA), alisema.

Imam Khomeini alisisitiza mifano bora kutoka kwa Seerah ya Bibi Zahra (SA) kama kielelezo cha kila kitu kwa ubinadamu na haswa kwa wanawake kufuata, aliongeza.

Mwanazuoni huyo aliendelea kusema kwamba Imam Khomeini aliitaja kumbukumbu ya kuzaliwa Bibi Zahra (AS) kuwa Siku ya Mwanamke Duniani kwa sababu binti huyu kipenzi wa Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) ni mfano wa kuigwa kwa wanawake wote.

Imam Khomeini alitaka wanawake wapate hadhi kama ile ya Bibi Zahra (SA) inayotokana na mafundisho ya Mwenyezi Mungu na uwepo wa Mwenyezi Mungu katika maisha na ni kwa kielelezo kama hicho ndipo uumbaji wa ustaarabu unaweza kupatikana, alisema.

Farhat pia alirejelea wazo la Imam Khomeini juu ya elimu kwa wanawake na akasema aliamini kwamba kujifunza ni ibada kwa wanaume na wanawake.

Muasisi huyo aliyefariki dunia wa Mapinduzi ya Kiislamu aliona fahari juu ya nafasi ambayo wanawake walikuwa nayo katika nyanja za elimu katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alibainisha.

Kwa mtazamo wa Imam Khomeini, wanawake wana nafasi muhimu kama mama na nguzo za familia katika kulea watoto waadilifu, aliongeza.

Kwa mujibu wa Farhat, Imam Khomeini pia alitilia maanani uwepo wa wanawake katika nyanja za kijamii na kisiasa na katika kuchangia maendeleo ya nchi yao.

Kwingineko katika matamshi yake, mwanazuoni huyo wa Algeria ametuma salamu za pongeza kwa munasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 45 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kuyataja kuwa ni ushindi kwa Umma mzima wa Kiislamu.

Taifa la Iran liliupindua utawala wa Pahlavi uliokuwa unaungwa mkono na Marekani Februari 11, 1979, na hivyo kuhitimisha miaka 2,500 ya utawala wa kifalme nchini.

Mapinduzi ya Kiislamu yaliyoongozwa na hayati Imam Khomeini yalianzisha mfumo mpya wa kisiasa unaozingatia maadili na demokrasia ya Kiislamu.

Wanawake wa Iran wamepata mafanikio makubwa tangu ushindi wa mapinduzi hayo. Wamepewa haki sawa kuunda mustakabali wao. Mapinduzi pia yaliwapa nafasi ya kujenga utambulisho wao wa kipekee wa kisiasa na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kufanya hivyo.

 

4198137

Habari zinazohusiana
captcha