Ulimwengu tunaoishi ni ule uliojaa harakati na shughuli za haraka na wakati mwingine tunaweza kujiuliza msukumo huu wote unahusu nini.
Ikiwa hatutajibu swali hili na badala yake kuendelea na uzembe au mghafala wetu, matendo na tabia zetu huelekea kwenye kutokuwa na maana na huwa upuuzi.
Kuna aya katika Qur'ani Tukufu inatuambia tuharakishe. Inalinganisha juhudi za watenda mema na mashindano ya kiroho ambayo lengo lake kuu ni kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu na baraka ya milele ya pepo.
Ni Aya ya 133 ya Surah Al Imran: “Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu.”
Kwa kuwa haiwezekani kufikia cheo cha kiroho bila ya kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kujitakasa na dhambi, lengo la mashindano haya ni kupokea kwanza Maghfira (msamaha wa kimungu) na pili kufikia pepo, ambayo ni kubwa kama mbingu na ardhi.
Kwa mujibu wa Tafsiri ya Qur'ani Tukufu ya Noor ya Hujjatul Islam Muhsin Qaraati, baadhi ya wanazuoni wanaamini kwamba pepo na moto tayari zipo na moja ya sababu zao za imani hii ni katika katika Qur'ani isemayo “iliyo wekwa tayari kwa wachamngu” katika aya hii.
Nukta nyingine katika aya hii ni kwamba kwa “Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi”, maana yake ni kuharakisha kutenda mema yenye kuleta msamaha wa Mwenyezi Mungu.
Katika tafsiri ya aya hii, Imam Ali (AS) alisema pitaneni katika kutekeleza majukumu yenu ambaye Mwenyezi Mungu amewaamurisha kuyafanya.
Ujumbe wa Aya ya 133 ya Surah Al Imran