IQNA

Shughuli za Qur'ani Tukufu

Zaidi ya wanafunzi 4,600 wanufaika mafunzo ya Qur’ani ya jumuiya ya misaada ya Kuwait

21:04 - December 29, 2022
Habari ID: 3476326
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Misaada ya Al-Najat ya Kuwait imesema zaidi ya wanafunzi 4,600 wamefaidika na programu zake za elimu ya Qur'ani Tukufu.

Jumuiya hiyo ilisema idara yake ya Qur'ani Tukufu na Seerah Nabawi imeandaa programu hizo.

Jaza al-Suwailah, afisa wa idara hiyo, alieleza kuwa ni mafanikio makubwa, akisema yamepatikana kutokana na uungaji mkono wa serikali ya Kuwait kwa mashirika ya misaada.

Amebainisha kuwa wavulana na wasichana 3,650 wamehudhuria programu za Qur'ani za mchana zinazofanywa na jamii na wengine 950 wamechukua kozi zinazofanyika nyakati za jioni.

Alisema mbinu za kisasa za ufundishaji zimetumika katika kozi hizo kwa lengo la kuwaongezea wanafunzi ujuzi wa Qur'ani Tukufu.

Kuwait ni nchi ya Kiarabu yenye Waislamu wengi katika eneo la Ghuba ya Uajemi ambako shughuli za Qur'ani Tukufu ni za kawaida sana.

4110268

captcha