IQNA

Hija 1444

Mahujaji waondoka Makka baada ya safari takatifu

21:18 - June 30, 2023
Habari ID: 3477218
Maelfu ya waumini Waislamu wanaendeea kuondoka katika mji mtakatigu wa Makka baada ya kumaliza ibada ya killa mwaka ya Hija ambayo mwaka huu imesadifiana na msimu wa joto kali.

Mwaka huu wa 1444 Hijria Qamaria sawa na 2023, waumini zaidi ya milioni 1.8 walishiriki katika Hajj, moja ya nguzo tano za Uislamu na moja ya mikusanyiko kubwa ya kidini ulimwenguni.

Siku ya Ijumaa, siku mbili baada ya ibada kuu ya mwisho, watu wengi walijaza barabara na mabasi ya kupanda ili kuondoka katika maeneo matakatifu huko Makka, na hivyo kuashiria kumalizika Ibada ya Hija. Kabla ya kuondoka, walitekeleza amali ya mwiso ya "Tawaf," wakizunguka Kaaba mara saba kwenye Msikiti mzuri wa Mecca.

Baadhi ya Mahujaji wataelekea nyumbani kwao, wakati wengine wataenda kwa Madina kuuzuru mji wa pili mtakatifu katika Uislamu uliko na Msikiti wa Mtume SAW unaojuikana kama Al-Masjid an-Nabawi.

Hija ilianza Jumatatu, Juni 26 na kumalizika Ijumaa, Juni 30. Mahujaji walifanya ibada mbali mbali kama kuzunguka Kaaba mara saba, wakitembea au kukimbia kati ya vilima vya Safa na Marwa, walisimama Kwenye Mlima Arafat, pia walitekeleza amali ya kumpiga mawe shetani, kuchinja, na kunyoa vichwa vyao.

Wakati Hajj ina historia ya changamoto mbali mbali, changamoto kuu ya mwaka huu ilikuwa joto kali.

Wakuu wa Saudia yaliripoti zaidi ya kesi 2,000 za dhiki ya joto, na joto likifikia nyuzi 48 Celsius wakati wa ibada ya Hija mwaka huu

Zaidi ya vifo 230 vilisajiliwa wakati wa Hajj mwaka huu, kimsingi kutoka Indonesia, wakati sababu maalum bado hazijatajwa.

Mahudhurio ya mwaka huu yalionyesha ongezeko kubwa kutoka mwaka uliopita wakati idadi ilipunguzwa kwa sababu ya janga la Covid-19.

/3484142

Hija mwaka imejiri katika katika msimu wa joto wa Saudia, sanjari na joto la jangwa linalosababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

captcha