IQNA

Uislamu Brazil

Waziri wa Utalii wa Brazil avaa Hijabu wakati akitembelea maonyesho ya Qur'ani

17:56 - June 04, 2023
Habari ID: 3477097
Waziri wa Utalii wa Brazil Daniela Carneiro ametembelea maonyesho ya Qur'ani Tukufu yanayoendelea katika nchi hiyo ya Amerika Kusini.

Carneiro, ambaye alikuwa amevalia vazi la staha la Kiislamu la Hijabu wakati wa ziara hiyo, alielezea maonyesho hayo kuwa ni tukio linalosaidia kuleta karibu dini pamoja.
Alisisitiza haja  ya kuyafanya maonyesho hayo kuwa  ya kudumu
Maonyesho ya Mus’haf Sharif yameandaliwa katika msikiti huko Foz do Iguaçu, mji ulio katika jimbo la Parana karibu na mipaka ya Argentina na Paraguay.
Wizara ya Masuala ya Kiislamu ya  Saudia imeandaa maonyesho hayo kwa ushirikiano na Kituo cha Kueneza Kiislamu cha Amerika Kusini.
Meya wa Foz do Iguaçu na maafisa wengine kadhaa waliandamana na waziri wa utalii katika ziara hiyo.
Mbali na nakala za Qur'ani Tukufu, maonyesho hayo yameonyesha shughuli za jumba la uchapishaji la Qur'ani mjini Madina pamoja na  programu za Qur'ani Tukufu.
Brazil ni nchi kubwa katika Amerika ya Kusini. Uislamu unafuatwa na zaidi ya Wabrazili 200,000—na kuifanya jumuiya kubwa zaidi ya Waislamu katika Amerika Kusini.
Wengi wa Waislamu wa nchi hiyo wana asili ya Waarabu, na idadi ndogo lakini inayoongezeka ya waongofu wa Brazili.
Jumuiya ya Waislamu wa Brazil inajumuisha Waislamu wa Sunni na Shia.

Brazil’s Tourism Minister Wears Hijab, Visits Quran Exhibition  

Brazil’s Tourism Minister Wears Hijab, Visits Quran Exhibition  

Brazil’s Tourism Minister Wears Hijab, Visits Quran Exhibition  


 
4145570

captcha