IQNA

Tangazo la Hija la Saudi Arabia

Mahujaji wanahitaji kupata chanjo ya 3 ya Corona siku 10 kabla ya Msimu wa Hija

16:45 - April 27, 2023
Habari ID: 3476922
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Hijja na Umra Saudi Arabia imesema kuwa tarehe ya mwisho ya Mahujaji kupata chanjo ni siku 10 kabla ya msimu wa Hija.

Kupata  chanjo ni sharti kila anayetaka kutekeleza ibada ya Hija mwaka huu wa 1444 Hijria au 2023.

Tangazo hilo limekuja kwa njia ya akaunti rasmi ya Twitter ya Wizara ya Hija na Umra ikiwa ni jibu kwa mtu mmoja aliyetaka maelezo. Mtu huyo alikuwa ameuliza ikiwa kupata chanjo ya tatu ya COVID-19 ni sharti la kuhiji.

Wizara ilifafanua kuwa kukamilisha chanjo zote ni lazima ili kupata kibali cha Hijja.

Utoaji wa kibali cha Hija mwaka huu utaanza tarehe 15 Shawwal, inayolingana na Mei 5, Wizara ilithibitisha.

Mwaka jana Saudia iliwapokea Mahujaji Waislamu kutoka nje ya nchi hiyo baada ya kusitishwa kwa miaka miwili lakini walipaswa kuwa wamepata chanjo tatu za COVID-19.

Chanjo ambazo Saudia mwaka jana ilikuwa imeziafiki ni pamoja na Pfizer-BioNTech (Comirnaty), Moderna (SpikeVax), AstraZeneca, Covishield, SK Bioscience, Vaxzevria, Jansen (Johnson & Johnson), na  Sputnik V. Chanjo zingine ambazo Saudia inazikubali lakini kwa masharti maalumu ni Sinopharm, Sinovac, na Covaxin. Mwaka huu pia Mahujaji wanatakiwa kufuatilia kupitia ofisi zao za kitaifa za Hija ili kupata maelezo kuhusu chanjo.

Hija ni safari ya kwenda Makka ambayo kila Mwislamu mwenye uwezo wa kimwili na uwezo wa kifedha anapaswa kuitekeleza angalau mara moja katika maisha yake.

3483339

Kishikizo: hija saudi arabia
captcha