IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya Iran

Hafidh wa Qur’ani kutoka Gambia apongeza usawa katika Mashindano ya Qur'ani ya Iran

22:29 - February 24, 2023
Habari ID: 3476617
TEHRAN (IQNA) – Hafidh wa Qur’ani Tukufu kutoka Gambia amesifu kiwango kizuri na usawa alioushuhudia katika Mashindano ya 39 la Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Iran.

Akizungumza na IQNA kando ya mashindano hayo yaliyofanyika Februari 18-22, Sheikh Tijan Salih aliyatathmini mashindano hayo kuwa "mazuri na ya shauku kubwa."

Duru hii ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani ilifanyika katika hatua mbili, ambapo duru ya kwanza ilifanyika kwa njia ya intaneti miezi kadhaa iliyopita na kushirikisha wagombea 150 kutoka nchi 80.

Kutoka miongoni mwao, maqari wa Qur'ani na waliohifadhi Qur'ani kutoka nchi 33 walifika kwenye fainali iliyofanyika mjini Tehran Februari 18-22. Mashindano hayo yalifunguliwa sambamba na mnasaba wa kukumbuka Kubaathiwa au kupewa utume, Mtume Muhammad SAW.

Kauli mbiu ya mashindano ya mwaka huu, kama lile lililotangulia, ni "Kitabu Kimoja, Umma Mmoja", jambo ambalo linaashiria Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inalipa umuhimu mkubwa umoja na udugu kati ya mataifa ya Kiislamu.

Shirika la Wakfu na Misaada la Iran kila mwaka huandaa mashindano ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu kwa kushirikisha wanaharakati wa Qur'ani Tukufu kutoka nchi mbalimbali.

captcha