IQNA

Kadhia ya Palestina

Al-Azhar: Msaada wa Waislamu kwa Msikiti wa Al-Aqsa ni kwa mujibu wa Imani za Kidini

20:44 - February 13, 2023
Habari ID: 3476558
TEHRAN (IQNA) - Afisa mwandamizi wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Misri amesema uungaji mkono kutoka kwa Waislamu kote ulimwenguni kwa Msikiti wa Al-Aqsa, al-Quds (Jerusalem) na Palestina unatokana na imani zao za kidini.

Akizungumza katika kongamano lililoandaliwa mjini Cairo na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Dola ya Palestina kuunga mkono al-Quds, Sheikh Mohamed al-Zuwaini alisema Mi'raj ya Mtukufu Mtume Muhammad (SAW) kutoka Msikiti wa Al-Aqsa ni sehemu ya imani za Waislamu.

Amesema Mwenyezi Mungu katika Qur'ani Tukufu ameunganisha Msikiti wa Al-Aqsa na Masjid al-Haram huko Makka na katika aya zinazofuata amezungumzia kuhusu ufisadi wa Bani Isra’il.

Amesema kuna haja ya Waislamu kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa ambao unakabiliwa na ufisadi wa Wazayuni.

Vile vile amesisitiza kuwa kukombolewa kwa Msikiti wa Al-Aqsa na kurudi kwake kwa Waislamu ni ahadi iliyomo ndani ya Qur'ani Tukufu na hakika itatokea.

Mkutano wa Kuunga mkono Jerusalem al-Quds ulianza Jumapili katika makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mjini Cairo kujadili uungaji mkono kwa Wapalestina wa al-Quds wanaoishi chini ya utawala wa kikoloni wa Israel.

Mkutano huo unaofanyika kwa ajili ya utekelezaji wa mapendekezo ya Mkutano wa hivi karibuni wa Algiers unalenga kuunga mkono na kuimarisha uthabiti wa wananchi wa Palestina wa Quds ambao wako mstari wa mbele kwa niaba ya mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kuulinda mji huo unaokaliwa kwa mabavu

4121719

captcha