IQNA

Muislamu wa Korea Kusini anatayarisha tarjuma ya Qur'ani Tukufu kwa Kikorea

12:40 - July 15, 2022
Habari ID: 3475505
TEHRAN (IQNA) – Lee Myung Won ni Muislamu kutoka Korea Kusini ambaye hivi sasa anafanya kazi ya kutafsiri Qur'ani Tukufu katika lugha ya Kikorea.

Won, ambaye alichukua jina la Ahmed baada ya kusilimu, anasema tarjuma ya kwanza ya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kikorea ilikamilika mwaka 1971 na mtarjumi alikuwa Yung Sung Kim na nyingine ilitolewa baadaye na Muislamu wa Korea.

Anasema kwamba tarjuma za sasa si sahihi sana na hazieleweki vyema.

Ahmed alisema ilimujia fikra ya tarjuma mpya Qur'ani Tukufu kwa lugha ya Kikorea ilimjia kwa mara ya kwanza alipofahamiana na mtaalamu wa Qur'ani na lugha ya Kiarabu wa Misri Ahmed Abdul Fattah Suleiman mwaka 1985.

Alisilimu baada ya kukutana na msomi huyo wa Kimisri na akajifunza Kiarabu kutoka kwake.

"Tangu wakati huo, nilikuwa nikifikiria kaundika tarjuma ya Qur'ani Tukufu," alisema na kuongeza, "Nilijifunza Qur'ani kwa miaka 30 ili kuielewa kikamilifu (kwa Kiarabu) kabla ya kuanza kutafsiri miaka mitatu iliyopita".

Ahmed alibainisha kuwa anatumia tafsiri nane za Qur'ani zilizoandikwa kwa lugha Kiarabu pamoja na tarjuma 13 za Kiingereza za Qur'ani Tukufu katika wakati anaandika tarjuma ya Kikorea.

Aidha anapanga pia kutayarisha tarjuma za vitabu kadhaa vya Hadith kwa Kikorea ili watu wa Korea Kusini wajifunze kuhusu utamaduni wa Kiislamu.

Kikorea ni lugha ya asili kwa watu wapatao milioni 80, wengi wao wakiwa wa asili ya Kikorea. Ni lugha rasmi na ya kitaifa ya Korea Kaskazini na Korea Kusini. Zaidi ya Korea, lugha hiyo ni lugha inayotambulika ya walio wachache katika sehemu za Uchina, yaani, Mkoa wa Jilin, na hasa Wilaya ya Yanbian na Kaunti ya Changbai. Pia inasemwa katika sehemu za kisiwa cha Urusi cha Sakhalin na sehemu za Asia ya Kati na Koryo-saram.

Katika Korea Kusini, Uislamu ni dini ya wachache. Jumuiya ya Waislamu iko mjini Seoul na kuna misikiti michache kote nchini.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Waislamu la Korea, kuna takriban Waislamu 100,000 wanaoishi Korea Kusini, takriban asilimia 70 hadi 80 kati yao ni wageni.

South Korean Muslim Convert Translating Quran into Korean

3479704

captcha