IQNA

Wananchi wa Iran wajitokeza kuadhimisha miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

11:08 - February 11, 2022
Habari ID: 3474915
TEHRAN (IQNA)-Wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leoi wamejitokeza kwa wingi mitaani katika maadhimisho ya miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini.

Leo Ijumaa tarehe 22 Bahman, sawa na tarehe 11 Februari, ni siku ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini (MA) mwaka 1979.

Katika sherehe hizo idadi kubwa ya wananchi wa taifa hili wamemiminika mabarabarani katika maandamano ya amani ya kumbukumbu ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu, ambapo kwa mara nyingine watajadidisha kiapo cha utiifu kwa Imamu Khomein, Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewataka wananchi wa Iran kujitokeza kushiriki katika maandamano ya maadhimisho ya miaka 43 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran sambamba na kulinda miiko ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Kutokana na janga la COVID-19, katika baadhi ya miji mijumuiko inafanyika kupitia misafara ya magari na pikipiki na katika baadhi ya miji kuna mijimuiko ya wananchi mitaani huku baadhi ya wananchi wakishiriki kwa njia ya kampeni katika mitandao ya kijamii.

Kadhalika Wairan watatangaza utiifu wao kwa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei.

Rais Ebrahim Raisi amesema kuwa, wananchi wa Iran wanapaswa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya leo ili kuwaonyesha walimwengu wote adhama na ukubwa wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imam Ruhullah Khomeini na kuhitimisha utawala utawala wa Shah uliokuwa ukiungwa mkono na madola ya Magharibi.

Ikumbukwe kuwa, miaka 43 iliyopita katika siku kama ya leo Iran ilikuwa katika siku ya kihistoria itakayokumbukwa siku zote. Siku hiyo wananchi waliokuwa wakipiga takbira na kutoa nara za kimapinduzi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi. Wananchi wanamapinduzi wa Iran, wanaume kwa wanawake, vijana kwa wazee na watu wa matabaka yote walisimama kidete wakipambana na mizinga na vifaru vya jeshi la Shah na kujisabilia kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiislamu. 

4035518

captcha