IQNA

Kuwait yaandaa mashindano ya Qur’ani ya mabingwa

21:57 - December 23, 2021
Habari ID: 3474714
TEHRAN (IQNA)- Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Kuwait imeandaa mashindano ya mabingwa wa Qur’ani katika kategoria za wanawake na wanaume.

Naibu Katibu wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Farid Emadi Jumatano alitangaza matokeo ya mashindano hayo yaliyopewa jina la ‘Safwat Al Awail’ ambayo yaliwashirikisha washindi wa mashindano yaliyopita ya Qur’ani nchini Kuwait.

Akizungumza katika hafla hiyo, Emadi amesema mashindano hayo ni ishara ya namna ambavyo Kuwait inavyoienzi Qur’ani Tukufu.

Kwa ujumla kulikuwa na washiriki 15 wanaume na 11 wanawake ambayo waliwahi kushika nafasi za kwanza katika mashindano yaliyopita ya Qur’ani Tukufu nchini humo.

Nafasi ya kwanza miongoni mwa wanawake ilishikwa na Taibah al Hindi aliyepata zawadi ya dola 26,400 naye Abdul Rahma Shuai ameshika nafasi ya kwanza miongoni mwa wanaume na pia amepata zawadi hiyo hiyo.

3477055

captcha