IQNA

Aya ya Qur'ani iliyopelekea Waislamu Uingereza kujiunga katika kampeni dhidi ya COVID-19

15:17 - August 12, 2021
Habari ID: 3474184
IQNA (TEHRAN)- Mafundisho ya Qur'ani Tukufu ndio chanzo cha Waislamu wengi nchini Uingereza kujitolea katika kampeni ya kukabiliana na janga la corona au COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa sehemu ya Aya ya 32 ya Sura Al Maida katika Qur'ani Tukufu isemayo: "Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote," imekuwa chanzo za Waislamu wa maeneo ya Birmingham na Black Country nchini Uingereza kujitolea kuwasaidia wengine wakati huu wa janga la COVID-19.

Kwa mujibu wa taarifa Waislamu katika maeneo hayo wamekuwa wakitumia misikiti na jumuiya zao kuwalisha, kuwalinda na kuwasaidia wasiojiweza katika jamii wakati huu wa janga la COVID-19.

Madaktari Waislamu pia wamekuwa katika mstari wa mbele kutoa huduma. Kwa mfano kundi la madaktari Waislamu linalojulikana kama Al Tabeeb Taskforce limekuwa likitoa mafunzo katika jamii kuhusu janga la COVID-19 kwa lugha mbali mbali.

Aidha wasomi wa Kiislamu pia wako mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu chanjo ya COVID-19. Sheikh Nuru Muhammad wa Kituo cha Kiislamu cha Al-Abbas amepongezwa kwa kufanikisha jitihada za kuhakikisha kuwa Waislamu waislamu wanachanjwa.

Mkakati huo wa Waislamu nchini Uingereza umeweza kuokoa maisha ya watu wengi na kuimarisha mshikamano katika jamii.

Jitihada hizo za Waislamu zime katika kitabu kipya kilichozinduliwa mwezi huu ambacho kimepewa jina la "Faith in Action-West Midlands Muslim Organizastion' COVID-19 response".

3990207/

captcha