IQNA

Waislamu Ethiopia wamiminika misikitini Mwezi wa Ramadhani

18:02 - July 07, 2015
Habari ID: 3325727
Waislamu katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa wamemiminika kwa wingi misikitini katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kiasi kwamba baadhi ya barabara zinafungwa kutoa nafasi ziada kwa wanaoswali.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu Ethiopia huukaribishwa  Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa raghba kubwa ya kidini. Imekuwa ni jambo la kawaida kwa Waislamu kujaa katika misikiti  na kupelekea barabara za kando kufungwa ili Waislamu waweze kupata nafasi ya kusimamisha ibada.
“Ethiopia  ina nafasi muhimu kama  nchi yenye wafuasi wa Uslamu, Ukristo na Uyahudi,” amesema Profesa Mohammed Zekeriya katika mahojiano na Shirika la Habari la Anadolu.  Zekeriya ni mshauri maalumu wa Taasisi ya Utafiti wa Ethiopia katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa.
“Ethiopia imetajwa katika vitabu vya Kiislamu kama eneo la kukimbilia na kupata hifadhi,” amesema. “Mtu wa kwanza aliyetamka takbir ya kwanza  katika mji mtakatifu wa Makka alikuwa, Bilal, Muethiopia.
Zekeriya amesema hiyo ni nukta inayoashiria uhusiano wa jadi baina ya watu wa Ethiopia na Bara Arabu.
“Mfalme wa Ethiopia alikuwa mkarimukwa wakimbizi wa kwanza Waislamu waliofika Abyssinia (Ethiopia) kwa amri ya Mtume Muhammad SAW,” amesema.
Waislamu wanakadiriwa kuwa takriabani asilimia 40 ya idadi ya watu milioni 94 nchini Ethiopia.../mh

3324001

captcha