IQNA

Ramadhani

Tafiti za Kisayansi Zafichua Faida za Kufunga

23:56 - April 06, 2024
Habari ID: 3478640
IQNA - Kufunga au saumu ni jambo la kawaida katika tamaduni na dini nyingi ulimwenguni kwa milenia.

Imezingatiwa kama tendo la ibada na njia ya matibabu. Madaktari mashuhuri kama vile Hippocrates, Pythagoras na Ibn Sina (Avicenna) waliponya baadhi ya magonjwa kwa kufunga.

Katika miongo ya hivi karibuni, idadi kubwa ya tafiti za kisayansi zimefanyika kuhusu faida  kufunga kula kwenye mwili wa binadamu. Tovuti ya Healthline yenye makao yake nchini Marekani imechapisha baadhi ya faida zilizothibitishwa kisayansi za kufunga.

Kulingana na tafiti, kufunga alfajiri hadi machweo kwa siku thelathini kiwango cha mwili kukataa insulini na huboresha udhibiti wa sukari katika damu. Kwa kweli, kwa kufunga, hutatua tatizo la insulin mwilini ambalo huwakumba watu wenye kisukari. Kiwango cha chini cha insulini husaidia glukosi kuhama kutoka kwenye damu hadi kwenye seli za mwili, jambo ambalo litapunguza kiwango cha sukari kwenye damu na kuzuia kisukari.

Kufunga pia husababisha kupunguzwa kwa alama za kuvimba, kichocheo kikuu cha magonjwa mengi sugu.

Utafiti mwingine wa watu wazima 110 waliofunga kwa wiki nne chini ya uangalizi wa madaktari ulionyesha matokeo mazuri ya kupungua shinikizo la damu pamoja na cholesterol na triglycerides. Kupungua huko huboresha afya ya moyo na kupunguza hatari ya kiharusi na mshtuko wa moyo.

Kwa kupunguza ulaji wa kalori na kuongeza kimetaboliki, kufunga husaidia watu kupoteza uzito. Tafiti nyingine zilizofanywa kwa watu wanaofunga zilionyesha kuwa viwango vya Homoni ya Ukuaji wa Binadamu (HGH) huongezeka kwa kufunga. Hii ina faida kwa kupoteza mafuta na kupata misuli, kwa kutaja machache.

Pia, tafiti katika panya zinaonyesha kuwa panya waliofunga walikuwa dhaifu, walikuwa na kumbukumbu bora na waliishi muda mrefu kuliko panya ambao hawakufunga.

Kufunga pia kuna uwezekano wa kusaidia kuzuia saratani na kupungza madhara ya tiba ya mionzi au chemotherapy.

Mbali na mchango wake katika afya ya mwili, funga ina faida nyingi za kiakili, kama vile kusaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuongeza ustahimilivu katika kukabiliana na mivutano na hali ngumu maishani.

3487783

captcha