IQNA

Uislamu Russia

Idadi ya Misikiti ya Russia imeongezeka mara 60 katika miongo mitatu

16:44 - December 14, 2023
Habari ID: 3478034
IQNA - Kumekuwa na ongezeko la rekodi la idadi ya misikiti nchini Russia (Urusi) katika miongo ya hivi karibuni, afisa mmoja alisema.

Akizungumza katika Kongamano la 19 la Kimataifa la Waislamu mjini Moscow mapema wiki hii, Magomedsalam Magomedov, naibu mkuu wa utawala katika Ofisi ya Rais wa Russia, alisema idadi ya misikiti imeongezeka mara 60 katika miongo mitatu.

Katika enzi ya Shirikisho la Sovieti, Uislamu ulidhibitiwa vikali, pamoja na dini nyingine zote, na idadi ya wahubiri wa Kiislamu waliotambuliwa rasmi ilikuwa ndogo. Shirikisho la Sovieti pia lilikuwa na idadi kubwa ya wahubiri wa Kiislamu wasiotambuliwa. Mnamo 1989,  vikwazo vingi dhidi ya Waislamu viliongolewa.

Baada ya Shirikisho la Sovieti kuanguka, uhuru wa kuabudu ukawa haki ya kikatiba nchini Russia ambayo ilishuhudia mwamko wa Kiislamu pamoja na dini nyinginezo, hasa Ukristo wa Othodoksi.

"Mnamo 1991, Russia ilikuwa na misikiti 120 tu inayofanya kazi na sasa idadi hiyo imeongezeka hadi zaidi ya 7,000," Magomedov aliambia kongamano hilo. "Kamwe katika historia yake taifa letu halijawahi kuona idadi kama hii," alibaini.

naibu mkuu wa utawala katika Ofisi ya Rais wa Russia pia alisema kwamba kila mwaka, Waislamu 25,000 wa Russia hushiriki katika ibada ya Hija nchini Saudia.

Moscow imetetea mara kwa mara maoni ya kidini ya Waislamu wakati kunaposhudiwa vipende vya kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu barani Ulaya.

Mwaka huu kumekuwepo na visa kadhaa vya wanaharakati kurarua hadharani nakala za Qur'ani Tukufu  haswa katika nchi za Nordic.

Akizungumzia vitendo hivyo, Rais Vladimir Putin alisema Qur'ani ni takatifu kwa Waislamu na inapaswa kuwa takatifu kwa wengine pia.

Akizungumza katika ziara yake huko Derbent katika Jamhuri ya Dagestan inayojiendesha ya Shirikisho la Russia mwezi Juni, aliongeza kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu sio jinai katika baadhi ya nchi bali ni jinai ambayo anayeitenda  nchini Russia ataadhibiwa.

"Katika nchi yetu, huu ni uhalifu kwa mujibu wa Katiba na kanuni ya adhabu," alisema.

"Siku zote tutafuata sheria hizi."

3486420

captcha