IQNA

Watetezi wa Qur'ani

Waislamu na Wakristo nchini Urusi walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu

18:21 - August 03, 2023
Habari ID: 3477374
MOSCOW (IQNA) – Mkutano wa shakhsia wa Kiislamu na Kikristo nchini Urusi (Russia) ulifanyika mjini Moscow kulaani vitendo vya hivi majuzi vya kufuru na kuilenga Qur'ani Tukufu barani Ulaya.

Mkutano huo ulifanyika Jumatano jioni kwa hisani ya Kituo cha Utamaduni cha Iran katika mji mkuu wa Urusi.

Waliohudhuria ni pamoja na balozi wa Iran nchini Urusi Kazem Jalali, makamu wa rais wa Muungano wa Waislamu wa Russia, mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Mashariki ya Chuo cha Sayansi cha Urusi, na katibu wa Kanisa la Othodoksi la Urusi na Mazungumzo ya Kidini.

Jalali katika hotuba yake alisema kuvunjiwa heshima Qur'anI Tukufu katika nchi za Magharibi kunakiuka Azimio la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (UDHR) pamoja na azimio la Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa na Ulaya.

Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Urusi, alisema kuchoma moto Qur'ani Tukufu ni sawa na hatua za makundi ya kigaidi yenye itikadi kali.

Amesema kuvunjiwa heshima Qur'ani katika nchi za Magharibi si jambo ambalo mtu anaweza kulipuuza kwa urahisi.

Damir Mukhetdinov, makamu wa rais wa Umoja wa Waislamu wa Russia katika hotuba yake amepongeza misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuwaunga mkono Waislamu wa dunia.

Pia alilaani kudhalilishwa kwa Qur'ani nchini Uswidi na Denmark na kusema haikubaliki kutukana matakatifu ya dini za Mwenyezi Mungu kwa kisingizio chochote, ikiwa ni pamoja na uhuru wa kujieleza.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mafunzo ya Mashariki ya Chuo cha Sayansi cha Urusi Ali Akbarov kisha akapanda jukwaa, akielezea kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu kkuwa ni mwendelezo wa mtazamo wa kikoloni wa Magharibi juu ya ulimwengu.

Mzungumzaji wa mwisho alikuwa Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Urusi Masoud Ahmadvand ambaye alisema hatua ya nchi za Magharibi kutoa ruhusa ya kuvunjiwa heshima Qur'ani inafichua ajenda yao dhidi ya Uislamu.

Ameongeza kuwa, badala ya kutumika kwa ajili ya kulinda maadili na ubinadamu, maneno muhimu kama vile uhuru wa kusema na uhuru wa dhamiri yamegeuka kuwa visingizio vya kukabiliana na kanuni hizo katika nchi za Magharibi.

 

4160005

Habari zinazohusiana
captcha