IQNA

Hija mwaka 1444

Maeneo matakatifu yatayarishwa kwa ajili ya Ibada ya Hija

19:23 - June 09, 2023
Habari ID: 3477125
Maeneo matakatifu nchini Saudi Arabia yanatayarishwa kupokea Waislamu wanaotekeleza ibada ya Hija kutoka kila kona ya dunia.

Kambi mpya zimetayarishwa na kuwekewa vifaa vya kutoa huduma zote muhimu ili kuhakikisha  Waislamu wanatekeleza ibada ya Hija bila matatizo. Kambi za viwango vya  juu zimejengwa ili kuzuia maafa ya moto  na halikadhalika viyoyozi katika  kila hema.

Meya wa mji mtakatifu waMakka ameanzisha vituo 28 vya huduma katika maeneo hayo matakatifu na kuwapa vifaa na nguvu kazi zinazohitajika kuwahudumia Mahujaji.

Huduma za afya na chakula pia hutolewa kwa mahujaji ambao idadi yao mwaka huu imepangwa kurudi katika viwango vyao vya kabla ya janga COVID-19.

Mamlaka za Saudia, zaidi ya hayo, zimezindua mtandao mrefu wa barabara zinazotumiwa na mahujaji kama sehemu ya maandalizi ya Hijja.

Makampuni yanayosimamia Mahujaji, kwa wakati huo, yamekamilisha kuandaa vituo vyao vya huduma  katika sehemu takatifu ndani na karibu na Makka, eneo takatifu zaidi katika Uislamu.

Hija, inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, ni moja ya ibada za wajibu katika Uislamu. Saudi Arabia imesema hakutakuwa na kikomo kwa idadi ya mahujaji kutoka kote ulimwenguni kwa msimu ujao wa Hija.

Inakadiriwa kuwa mwaka huu, Saudi Arabia itapokea Mahujaji zaidi ya milioni mbili, kiasi kwamba mashirika ya ndege ya nchi hiyo yameshatenga tiketi zaidi ya 1,200,000 kwa ajili ya wageni wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu. Viwanja sita vya ndege vya ndani ikiwa ni pamoja na Jeddah, Riyadh, Al-Dammam, Madinatul-Munawwara, Al-Taif na Yan'ba vitapokea ndege zitakazobeba mahujaji wa mwaka huu.

3483867

captcha