IQNA

Waislamu Kanada

Polisi Kanada walaaniwa kwa kutumia mabavu kumkamata Mwislamu mwenye asili Afrika

18:16 - April 28, 2023
Habari ID: 3476926
TEHRAN (IQNA) - Shirika moja la Waislamu wa Kanada (Canada) limelaani hatua ya polisi wa Edmonton ya kumkamata kwa mabavu na vurugu Mwislam mwenye asili ya Afrika wiki iliyopita.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano, Shirika la Waislamu Kanada (NCCM) lilisema mtu huyo, ambaye hajatajwa kulinda faragha yake na ya familia yake, alikuwa akiendesha gari kutoka msikiti wa Edmonton Kusini mnamo Aprili 21 baada ya kushiriki katika sala ya Ijumaa.

Mtu huyo, ambaye alikuwa amevalia kanzu na kilemba, alikuwa akiendesha gari na mke wake na watoto wadogo ndani. Alisimamishwa a polisi wa Edmonton kwa kuripotiwa kwenda kasi ya kilomita 47 kwa saa katika eneo la kilomita 30 kwa saa.

Polisi wa Edmonton, katika taarifa Jumatano, walithibitisha kwamba ilitolewa karibu saa nane unusu. Aprili 21 maafisa walikuwa katika doria ya kudhibiti kasi kwenye Barabara ya Millwoods kati ya 36 Avenue na 36B Avenue wakati wa tukio hilo.

Shirika hilo la Waislamu lilisema mtu huyo aligundua kuwa mmoja wa maafisa alionekana mwenye hasira na hivyo alitaka afisa wa ngazi za juu awepo kabla ya kupeana leseni ya dereva na kitambulisho. Kisha akatolewa ndani ya gari na mmoja wa maafisa aliweka goti lake juu ya kwenye shingo yake.

Uchunguzi kuhusu kesi hiyo unaendelea ili kuhakikisha kuwa matukio kama hayo hayakaririwi tena.

3483347

Kishikizo: kanada waislamu
captcha