IQNA

Ujumbe wa Siku ya Kimataifa ya Quds

Wizara ya Mambo ya Nje Iran yaitaka jamii ya kimataifa kukomesha jinai za Israel

14:16 - April 13, 2023
Habari ID: 3476862
TEHRAN (IQNA)-Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekumbusha wajibu wa kisheria wa mashirika na taasisi za kimataifa na za kutetea haki za binadamu wa kuunga mkono haki za watu walio chini ya utawala ghasibu huko Palestina, na kutoa wito wa kukomeshwa uvamizi huo na kusimamisha jinai za Wazayuni.

Wito huo umetolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika taarifa yake kwenye mkesha wa Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iliyotolewa kwa mnasaba wa Siku ya Quds Duniani, imeeleza kuwa, hivi sasa Palestina na Quds Tukufu zimekuwa nembo ya umoja wa Ulimwengu wa Kiislamu na nembo ya kupigania haki za watu wanaodhulumiwa na wapigania uhuru wa watu wa rangi, dini na madhehebu zote.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa: Kilio cha kudhulumiwa taifa la Palestina na hakika ya yanayojiri katika ardhi ya Palestina vitasikika zaidi katika Siku ya Quds mwaka huu kuliko wakati mwingine wowote kutoka kwenye vinywa vya mamia ya mamilioni ya watu wanaopigania haki na uhuru duniani kote. Imesema hii leo  Palestina sio tu kadhia ya kwanza la Ulimwengu wa Kiislamu, bali pia mfano wa wazi zaidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, sheria na kanuni za kimataifa.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran inasema: Kama alivyosema Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, siasa kuu za ubeberu na Uzayuni ni kufifiza suala la Palestina katika fikra za jamii za Kiislamu na kulisahaulisha.

Taarifa hiyo inaongeza kuwa: Wakati magaidi wa Kizayuni wameua shahidi Wapalestina wapatao mia moja wakiwemo watoto na wanawake katika miezi mitatu tu ya mwanzo ya mwaka mpya pekee, Wamagharibi wanaodai kutetea haki za binadamu na waungaji mkono wa utawala ghasibu wa Israel hususan Marekani na nchi kadhaa za Ulaya, wamekuwa wafadhili wakubwa zaidi wa ugaidi kwa kuendelea kukaa kimya mbele ya uhalifu huu.

Taarifa ya Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran imeeleza kuwa: Katika siku za hivi karibuni, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameuvunjia heshima Msikiti wa Al-Aqswa, kibla cha kwanza cha Waislamu duniani, na kumwaga damu za waumini waliokuwa katika ibada ya Itikafu ndani ya msikiti huo' na kwa mara nyingine wameonyesha sura halisi na mbaya ya utawala huo wa kibaguzi mbele ya ulimwengu.

Imam Khomeini MA mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alitangaza Ijumaa ya mwisho ya mwezi Mtukufu wa Ramadhani kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds. 

Waislamu na wapenda haki kote duniani wamekuwa wakifanya maandamano katika kila mwaka katika Siku ya Kimataifa ya Quds, na kuonyesha hasira zao dhidi ya siasa za kibaguzi za Israel na mshikamano wao na wananchi madhulumu wa Palestina.

Siku ya Kimataifa ya Quds mwaka huu itafanyika Ijumaa ya kesho tarehe 23 Ramadhani 1444.

/3483185

 

3483185

captcha