IQNA

Mawaidha

Waumini wa kweli hawakai kimya mbele ya dhulma

22:21 - April 05, 2023
Habari ID: 3476816
TEHRAN (IQNA) – Muumini wa kweli si yule anayefikiria tu kuhusu mambo ya kiroho kwa sababu muumini wa kweli hawezi kuwa mwenye kutojali ukiukwaji wa haki za wengine.

Katika mfululizo wa darsa mwalimu wa vyuo vya Kiislamu Hujjatul Islam Mohammad Soroosh Mahallati hutoa maelezo kuhusu Du'a al-Sahar, pia inajulikana kama Du'a al-Baha. Waislamu wameshauriwa kusoma dua hiyo katika alfajiri ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hapa anafafanua sehemu moja ya dua hiyo isemayo: “Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba unipe kutoka katika nuru Yako kwa mwangaza wake wa juu kabisa, na Nuru Yako yote ni yenye kung’aa. Ewe Mwenyezi Mungu, nakuomba kwa Nuru yako yote.”

Suala la nuru ya Mwenyezi Mungu limetajwa katika riwaya nyingi. Nuru iliyotajwa katika dua hii inaashiria ukamilifu wa nuru ya Mwenyezi Mungu; hii ina maana kwamba mtu anaweza kuona mwanga huu katika kila kiumbe na kitu.

Haki ni nuru na uonevu au dhulma  ni giza

Ukandamizaji, uonevu, na dhulma huandamana na giza; palipo na dhuluma, pana giza na popote palipo na giza, kuna uonevu.

Aya za Qur'ani Tukufu zinazotuita kukaribia nuru kwa hakika zinatutaka tuondoe dhulma na kuweka nuru (haki) badala yake.

Aya ya 69 ya Surah Az-Zumar inasema: “ Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa baina yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa.”

Nuru hapa hairejelei nuru tunayoiona kwa macho. Kulingana na mwanafalsafa na mfumbo Mohsen Fayz Kashani, kuangaza kwa nuru duniani kutatokea wakati haki itakapothibitishwa. Mwenyezi Mungu ameitaja haki kuwa nuru. Miji yote inapopambwa kwa haki na haki za watu zinaheshimiwa, jamii huangaza zaidi.

captcha