IQNA

Waislamu Kanada

Mashindano ya Qur'ani yamepangwa kufanyika Alberta nchini Kanada

19:56 - December 31, 2022
Habari ID: 3476337
TEHRAN (IQNA) - Jumuiya ya Waislamu wa Kanada (MAC) itaandaa mashindano yake ya 20 ya Qur'ani Tukufu Januari Mosi 2023.

Shindano hilo litafanyika ana kwa ana na washiriki watashindana katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu, kulingana na tovuti ya MAC.

Wale waliozaliwa kati ya 2004 na 2018 wanaweza kushiriki katika sehemu ya vijana ya mashindano hayo ya Qur'ani Tukufu.

Kila mshindani anaweza kushindana katika kategoria moja ya shindano pekee.

Jumuiya ya Waislamu ya Kanada, kulingana na tovuti yake, ni shirika la misaada la Kanada na vuguvugu la kijamii la mashinani.

Inalenga kuwahudumia Wakanada kwa kuwaelimisha na kuwatia moyo Waislamu nchini Kanada kuwawezesha kutekeleza imani yao kwa vitendo kwa manufaa ya kila mtu.

Ofisi kuu ya MAC huko Edmonton, Alberta, inajumuisha msikiti, shule ya Kiislamu na vituo viwili vya vijana. Jumuiya hiyo ina ofisi katika miji 13 ya Kanada.

4110802

captcha