Hafla ya uzinduzi ilifanyika Alhamisi katika Msikiti wa Mfalme Salman. Katika hafla hiyo, makamu wa rais pia alifungua tamasha la "Mahrajan Al-Quran" kwenye uwanja wa msikiti.
Akizungumza katika hafla hiyo, alisisitiza kuwa serikali ya Maldives inalipa umuhimu suala la kueneza elimu ya Qur'ani Tukufu na Uislamu kwa ujumla.
Akiangazia idadi inayoongezeka ya watoto wanaohifadhi Qur'ani Tukufu na kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya usomaji Qur’ani, Naseem alitoa shukurani zake kwa Kituo cha Kitaifa cha Qur’ani Tukufu, walimu na wazazi.
Zaidi ya hayo, makamu wa rais alihimiza kila mtu kukariri Kurani Tukufu mara nyingi iwezekanavyo, kujifunza kuelewa maana yake, na kujitahidi kufuata mafundisho ya Kitabu hicho Kitakatifu.
Jumla ya wanafunzi 1,023 wanashiriki katika kategoria tatu za Mashindano ya 35 ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur'ani.
Maldives au Maldivi ni nchi huru kwenye funguvisiwa la Maldivi katika Bahari Hindi katika eneo la kusini mwa Asia. Nchi hiyo inajumuisha visiwa 1,192 na kati ya hivyo takriban 200 hukaliwa na watu. Idadi ya watu katika nchi hiyo ndogo inakadiriwa kuwa nusu milioni na asilimia 100 ya raia wa nchi hiyo ni Waislamu.
3481794