IQNA

Watawala wa Saudia na Kuwait walazwa hospitalini

15:06 - July 20, 2020
Habari ID: 3472981
TEHRAN (IQNA) – Mfalme Salman wa Saudi Arabia amelazwa hospitalini katika mji mkuu wa nchi hiyo, Riyadh kutokana na matatizo ya kibofu cha nyongo.

Taarifa ya Kasri ya Ufalme imesema mfalem huyo mwenye umri wa miaka 84 anapata matibabu katika Hospitali ya Kitaalamu ya Mfalme Faisal. Hakuna maelezo zaidi yaliyotolewa kuhusu hali ya kiafya ya mfalme huyo.

Hospitali ya Kitaalamu ya Mfalme Faisal huwa inatoa matibabu kwa wanawafalme wa Saudia na katika miezi ya hivi karibuni imekuwa ikitoa matibabu kwa wale walioambukizwa corona.

Mfalme Salman aliingia madarakani Januari 2015 na anatazamiwa kuwa mfalme wa mwisho wa kizazi cha mandugu zake ambao wamekuwa madarakani baad aya kifo cha baba yao, na muasisi wa Saudia, Mfalme Abdulaziz.

Mfalme Salman amempa mamlaka makubwa mwanae mwenye umri wa miaka 34, Mohammad bin Salman ambaye ndiye mrithi wa kiti cha ufalme. Bin Salman ambaye ni maarufu kama MBS anatazamwa kama mtu mwenye kiburi na anatumia vibaya madaraka kuwakandamiza wale ambao wanaonekana kupinga mpango wake wa kutwaa madaraka.

Kwingineko siku ya Jumapili Amir wa Kuwait Sabah al-Ahmad al-Jaber al-Sabah, 91, naye siku ya Jumapili alifanyiwa upasuaji 'uliofanikiwa' baada ya kulazwa hospitalini Jumamosi.

3472045

captcha