Kiongozi Muadhamu wa Mapiduzi ya Kiislamu ya Iran amesema imani kwa Mwenyezi Mungu na kumkufuru taghuti ni
msingi wa asili na wa kweli wa nguvu, na huku akisisitiza kwamba
Marekani ni "taghuti mkuu" na ni
"shetani mkubwa". Ameongeza kuwa leo wadhifa na
jukumu muhimu zaidi la maulama, wanafikra na wasomi ni kufafanua mambo
na kufanya jihadi ya mwamko katika kukabiliana na hila za mataghuti na
kuutaka Umma wa Kiislamu pia usihadaike na hila hizo wala kutishwa na
vitisho vyao. Huku akiwashukuru waandaaji na wasimamizi wa mashindano
haya ya Qur’ani, Kiongozi Muadhamu amesema kuwa Qur’ni ni muhimili wa
umoja kati ya Umma wa Kiislamu na kuongeza kuwa katika hali ambayo siasa
za uistikbari zimesimama kwenye msingi wa kuleta hitilafu na mivutano
kati ya Waislamu, Umma wa Kiislamu unapasa kushikamana na neema hiyo
kubwa ya Mwenyezi Mungu katika kufuata njia ya umoja na mshikamano.
Ayatullah Khamanei amesema kuwa moja ya baraka za vikao vya Qur’ani ni
kufarijika matabaka mbalimbali ya watu na hasa tabaka la vijana na
kuongeza: Umma wa Kiislamu hii leo unahitajia mafudisho, fikra na
maarifa ya Qur’ani kuliko wakati mwingine wowote kwa sababu hali halisi
ya maisha ya Waislamu iko mbali sana na Qur’ani. Huku akiashiria juhudi
kubwa zinazofanywa na madola ya kitaghuti kwa ajili ya kutoa pigo dhidi
ya Uislamu na Umma wa Kiislamu, Ayatullah Khamenei amesema: Wao
wanafahamu vyema kuwa iwapo Waislamu watapata nguvu na sauti yao
kusikika na kuwa kubwa, bila shaka hawataweza tena kuyadhulumu mataifa
na suala la Palestina kwa maana ya kughusubiwa taifa la Kiislamu
litaondoka na kusahaulika kabisa.
Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu
amesema siri ya kuvunjwa njama hizo ni kushikamana kikamilifu na Qur’ani
Tukufu na kupata misingi halisi ya nguvu. Ameongeza kuwa nguvu halisi
inapatikana katika imani, kusimama imara na kukufuru taghuti. Huku
akielezea masikitiko yake kuhusiana na hatua ya baadhi ya nchi ya
kushikamana na taghuti badala ya Mwenyezi Mungu, Ayatullah Khemeni
amesisitiza kwamba nchi ambazo zinatekeleza siasa za Marekani katika
eneo kwa hakika zinafanya hiana dhidi ya Umma wa Kiislamu na kuandaa
uwanja wa Marekani kupenya zaidi katika eneo. Amesema, imani na uthabiti
wa taifa la Iran na mapambano yake katika kukabilian ana matakwa ya
ziada ya Marekani ndicho chanzo halisi cha nguvu ya Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran na kusisitiza kwamba sababu ya madola makubwa kuliogopa taifa la
Iran na kutekelezwa njama tofauti dhidi ya taifa hili ni nguvu yake
iliyosimama juu ya msingi wa Uislamu na kwamba bila shaka adui anauogopa
Uislamu wenye nguvu na ulio shujaa. Huku akisisitiza kwamba misimamo na
utendaji wenye nia nzuri wa Iran ndicho chanzo cha kuwa na athari na
ushawishi wa nchi hii miongoni mwa Waislamu na sababu nyingine ya nguvu
na uwezo mkubwa wa Mfumo wa Kiislamu, Ayatullah Khamenei amesema kuwa si
ahadi za mataghuti zimeweza kulihadaa taifa la Iran wala vitisho vyao
kulifanya liogope. Ayatullah Khamanei amesema kuwa moja ya mahitaji
muhimu ya ulimwengu wa Kiislamu ni kutohadaika na ahadi za madola
makubwa na pia kutoogopa vitisho vyao. Ameongeza kuwa hii leo wadhifa na
jukumu muhimu zaidi la watu wote kwenye Umma wa Kiislamu na hasa
maulamaa, wanafikra na wasomi wa nchi za Kiislamu ni mapambano kwa ajili
ya kuleta mwamko na jihadi ya ufafanuzi wa mambo kuhusiana na uhalisi
wa mambo katika ulimwengu wa Kiislamu. Amesema kudhihiri kwa makundi ya
kigaidi na kitakfiri katika eneo na kuzua vita na hitilafu miongoni mwa
Waislamu kwa niaba ya maadui ni nitija ya upotovu na kutokuwa na mwamko
na kusema: Vikao vya Qur’ani vinapasa kutumika kwa ajili ya kuleta
mwamko na watu wanaoshiriki kwenye vikao hivi kutoka nchi mbalimbali
wanapasa kuongoza na kuleta utambuzi wa mambo katika nchi zao. Huku
akisisitiza kuwa msaada na nusra ya Mwenyezi Mungu inatokana na harakati
ya mataifa ya Kiislamu ambayo nayo (harakati hiyo) inatokana na jihadi
ya mwamko. Kiongozi Muadhamu amesema kuwa hakuna shaka kwamba hatimaye
mrengo wa kufri utalazimika kusalimu amri mbele ya mrengo wa Uislamu wa
mapambano na wa jihadi.
Kabla ya hotuba ya Kiongozi Mudhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu, Hujjatul Islam wal Muslimeen Muhammadi,
Mwakilishi wa Kiongozi Muadhamu ambaye pia ni Mkuu wa Taasisi ya Wakfu
na Masuala ya Kheri, amesema kuwa kaulimbiu ya duru hii ya 33 ya
mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu ilikuwa ni ‘Kitabu Kimoja,
Taifa Moja’ ambapo washiriki 130 kutoka nchi 70 za dunia wameshiriki
katika vitengo vya hifdhi na kiraa ya kitabu hicho kitakatifu. Huku
akiwaenzi mashahidi wa maafa ya Mina na hasa mashihidi wa Qur’ani Tukufu
Hujjatul Islam wal Muslimeen Muhammadi amesema kuwa mahudhurio ya
kwanza ya wasomaji Qur’ani wasio na uwezo wa kuona kutoka nchi tofauti
katika mashindano hayo, kuenziwa kwa familia za mashahidi wa Qur’ani na
mashahidi wa kulindwa Haram ya Bibi Zeinab (as) huko Damscus Syria,
kuwasilishwa kwa makala na utafiti wa Qur’ani pamoja na kufanyika
maonyesho na vikao vya Qur’ani ni miongoni mwa shughuli zilizotekelezwa
katika duru hii ya 33 ya mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu.
3499266